Surah Al-Insaan — Man
Surah Al-Insaan (Man) — 76/114 · 31 aya. Soma na usikilize kwa maandishi ya Kiarabu na tafsiri ya Kiswahili.
هَلۡ أَتَىٰ عَلَى ٱلۡإِنسَٰنِ حِينࣱ مِّنَ ٱلدَّهۡرِ لَمۡ يَكُن شَيۡـࣰٔ ا مَّذۡكُورًا
Kishampitia binadamu kipindi kirefa cha wakati kabla hajapulizwa roho ambapo hakuwa ni kita kinachotajika wala haijulikani athari yake
Ayah 1إِنَّا خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ مِن نُّطۡفَةٍ أَمۡشَاجࣲ نَّبۡتَلِيهِ فَجَعَلۡنَٰهُ سَمِيعَۢا بَصِيرًا
Sisi tumemuumba binadamu kutokana na tone la manii la mchanganyiko wa maji ya mwanamume na maji ya mwanamke, ili tumtahini kwa lazima za kisheria baadaye, hivyo basi tumfanya ni mwenye masikio ya kusikia na macho ya kuonea, apate kuzisikia aya na kuziona dalili
Ayah 2إِنَّا هَدَيۡنَٰهُ ٱلسَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرࣰ ا وَإِمَّا كَفُورًا
Sisi tumembainishia na kumfahamisha njia ya uongofu na upotevu na wema na ubaya ili awe ima ni mwenye kuamini na kushukuru. Au awe ni mwenye kukanusha na kukataa
Ayah 3إِنَّآ أَعۡتَدۡنَا لِلۡكَٰفِرِينَ سَلَٰسِلَاْ وَأَغۡلَٰلࣰ ا وَسَعِيرًا
Sisi Tumewaandalia wakanushaji pingu za chuma za kuifunga miguu yao na minyororo ya kufungiwa mikono yao hadi shingo zao na moto ambao watachomwa nao
Ayah 4إِنَّ ٱلۡأَبۡرَارَ يَشۡرَبُونَ مِن كَأۡسࣲ كَانَ مِزَاجُهَا كَافُورًا
Hakika watu wa utiifu na ukweli wa Imani wanaotekeleza haki za Mwenyezi Mungu, watakunywa, Siku ya Kiyama, kutoka kwenye kikombe ambacho ndani yake mna Pombe lililochanganywa na aina bora kabisa ya harufu nzuri, nayo ni maji ya kafuri
Ayah 5عَيۡنࣰ ا يَشۡرَبُ بِهَا عِبَادُ ٱللَّهِ يُفَجِّرُونَهَا تَفۡجِيرࣰ ا
Kinywaji hiki kilichochanganywa na kafuri, ni chemchemi wanayokunywa waja wa Mwenyezi Mungu, wanaitumia na kuipitisha wanavyotaka mapitisho mazuri
Ayah 6يُوفُونَ بِٱلنَّذۡرِ وَيَخَافُونَ يَوۡمࣰ ا كَانَ شَرُّهُۥ مُسۡتَطِيرࣰ ا
Hao walikuwa huko duniani wanatekeleza kile walichojilazimisha nafsi zao cha utiifu kwa Mwenyezi Mungu, na wakiogopa mateso ya Mwenyezi Mungu, Siku ya Kiyama, ambayo madhara yake ni hatari na ubaya ni wenye kusambaa na kuenea kwa watu isipokuwa wale ambao Mwenyezi Mungu Amewarehemu
Ayah 7وَيُطۡعِمُونَ ٱلطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِۦ مِسۡكِينࣰ ا وَيَتِيمࣰ ا وَأَسِيرًا
Na wanalisha chakula, pamoja na kuwa wanakipenda na kukihitajia, kumpa fukara asiyeweza kuchuma, asiyemiliki chochote katika vitu vya kilimwengu, na kumpa mtoto aliyefiliwa na babake kabla ya kubaleghe na asiye na mali, na kumpa mtu aliyetekwa vitani miongoni mwa washirikina na wengineo
Ayah 8إِنَّمَا نُطۡعِمُكُمۡ لِوَجۡهِ ٱللَّهِ لَا نُرِيدُ مِنكُمۡ جَزَآءࣰ وَلَا شُكُورًا
na huku wanasema katika nafsi zao, «Hakika sisi tunawafanyia wema kwa kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu na kutaka malipo yake. Hatutaki badala wala hatukusudii kushukuriwa wala kusifiwa na nyinyi
Ayah 9إِنَّا نَخَافُ مِن رَّبِّنَا يَوۡمًا عَبُوسࣰ ا قَمۡطَرِيرࣰ ا
Kwa kweli, sisi tunaiogopa, kutoka kwa Mola wetu, Siku ngumu ambayo ndani yake nyuso zitakunjana na mapaji yatasinyaa kutokana na mambo yake mazito na vituko vyake vikubwa
Ayah 10فَوَقَىٰهُمُ ٱللَّهُ شَرَّ ذَٰلِكَ ٱلۡيَوۡمِ وَلَقَّىٰهُمۡ نَضۡرَةࣰ وَسُرُورࣰ ا
Basi hao Mwenyezi Mungu Atawaokoa na shida za Siku hiyo na Atawapa uzuri na mwangaza katika nyuso zao na furaha ndani ya nyoyo zao
Ayah 11وَجَزَىٰهُم بِمَا صَبَرُواْ جَنَّةࣰ وَحَرِيرࣰ ا
na Atawalipa, kwa kuvumilia kwao duniani juu ya utiifu, Pepo iliyo kubwa ambayo kutoka humo watakula wanachokitaka na watavaa humo hariri nyororo
Ayah 12مُّتَّكِـِٔينَ فِيهَا عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِۖ لَا يَرَوۡنَ فِيهَا شَمۡسࣰ ا وَلَا زَمۡهَرِيرࣰ ا
hali ya kuwa wametegemea juu ya vitanda vilivyopambwa kwa nguo na pazia za fahari. Hawataona humo joto la jua wala ukali wa baridi
Ayah 13وَدَانِيَةً عَلَيۡهِمۡ ظِلَٰلُهَا وَذُلِّلَتۡ قُطُوفُهَا تَذۡلِيلࣰ ا
Na karibu nao, kutakuwa na miti ya Pepo yenye kuwafinika ambayo wamerahisishiwa kuyachuma matunda yake
Ayah 14وَيُطَافُ عَلَيۡهِم بِـَٔانِيَةࣲ مِّن فِضَّةࣲ وَأَكۡوَابࣲ كَانَتۡ قَوَارِيرَا۠
Watawazunguka wao watumishi wakiwa na vyombo vya vyakula vya fedha, na vikombe vya vinywaji vya ukoa
Ayah 15قَوَارِيرَاْ مِن فِضَّةࣲ قَدَّرُوهَا تَقۡدِيرࣰ ا
ukowa wa fedha, ambavyo wanyweshaji wamevima kadiri ya watakavyotamani wenye kunywa, haviongezeki wala havipungui
Ayah 16وَيُسۡقَوۡنَ فِيهَا كَأۡسࣰ ا كَانَ مِزَاجُهَا زَنجَبِيلًا
Na watu wema hawa watanyweshwa Peponi kikombe kilichijazwa Pombe iliyochanganywa na tangawizi
Ayah 17عَيۡنࣰ ا فِيهَا تُسَمَّىٰ سَلۡسَبِيلࣰ ا
watakunwa kutoka kwenye chemchemi iliyoko Peponi inayoitwa Salsabīl, kwa kuwa kinywaji chake kina usalama na kuwa kina ulaini na ladha ya kupendeza
Ayah 18۞وَيَطُوفُ عَلَيۡهِمۡ وِلۡدَٰنࣱ مُّخَلَّدُونَ إِذَا رَأَيۡتَهُمۡ حَسِبۡتَهُمۡ لُؤۡلُؤࣰ ا مَّنثُورࣰ ا
Na watawazunguka wema hawa wakiwatumikia wavulana wenye hali moja ya kudumu, ukiwaona utawadhania, kwa uzuri wao na usafi wa rangi zao na mng’aro wa nyuso zao, kuwa ni lulu iliyotenganishwa inayong’ara
Ayah 19وَإِذَا رَأَيۡتَ ثَمَّ رَأَيۡتَ نَعِيمࣰ ا وَمُلۡكࣰ ا كَبِيرًا
Na utazamapo mahali popote katika Pepo utaona starehe isiyosifika na ufalme mkubwa uliop mkunjufu usiosiokuwa na mwisho
Ayah 20عَٰلِيَهُمۡ ثِيَابُ سُندُسٍ خُضۡرࣱ وَإِسۡتَبۡرَقࣱۖ وَحُلُّوٓاْ أَسَاوِرَ مِن فِضَّةࣲ وَسَقَىٰهُمۡ رَبُّهُمۡ شَرَابࣰ ا طَهُورًا
Juu ya miili yao pana nguo zilizoipamba, ambazo sehemu zake za ndani kuna hariri nyembamba ya rangi ya kijani, na nje yake kuna hariri nene. Na miongoni mwa mapambo watakayovishwa ni makuku ya fedha. Na Mola wao Atawanywesha, juu ya sterehe hizo, kinywaji kisicho na uchafu wala rojo
Ayah 21إِنَّ هَٰذَا كَانَ لَكُمۡ جَزَآءࣰ وَكَانَ سَعۡيُكُم مَّشۡكُورًا
Na wataambiwa, «Hakika nyinyi mmetayarishiwa haya yakiwa ni badala ya matendo yenu mema, na matendo yenu duniani yalikuwa ni yenye kukubaliwa na kuridhiwa na Mwenyezi Mungu.»
Ayah 22إِنَّا نَحۡنُ نَزَّلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡقُرۡءَانَ تَنزِيلࣰ ا
Hakika sisi tumekuteremshia Qur’ani, ewe Mtume, materemsho yanayotoka kwetu, ili uwakumbushe watu yale yaliyomo ndani ya maagizo mema, matahadharisho ya ubaya, malipo mazuri na mateso
Ayah 23فَٱصۡبِرۡ لِحُكۡمِ رَبِّكَ وَلَا تُطِعۡ مِنۡهُمۡ ءَاثِمًا أَوۡ كَفُورࣰ ا
Basi yavumilie maamuzi ya Mola Wako Aliyokupangia na uyakubali, na usonge mbele kufuata maamrisho yake ya Kidini, na usiwatii washirikina waliovama kwenye matamanio au waliokolea kwenye ukafiri na upotevu
Ayah 24وَٱذۡكُرِ ٱسۡمَ رَبِّكَ بُكۡرَةࣰ وَأَصِيلࣰ ا
na uendelee kutaja jina la Mola wako na kumuomba mwanzo wa mchana na mwisho wake
Ayah 25وَمِنَ ٱلَّيۡلِ فَٱسۡجُدۡ لَهُۥ وَسَبِّحۡهُ لَيۡلࣰ ا طَوِيلًا
Na wakati wa usiku, mnyenyekee Mola wako na umswalie na umuabudu kipindi kirefu cha usiku
Ayah 26إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ يُحِبُّونَ ٱلۡعَاجِلَةَ وَيَذَرُونَ وَرَآءَهُمۡ يَوۡمࣰ ا ثَقِيلࣰ ا
Kwa hakika hawa washirikina wanaupenda ulimwengu na wanaushughulikia, na wanakuacha nyuma ya migongo yao kule kufanya matendo ya kuwafaa Akhera na kuwaokoa katika Siku yenye shida kubwa
Ayah 27نَّحۡنُ خَلَقۡنَٰهُمۡ وَشَدَدۡنَآ أَسۡرَهُمۡۖ وَإِذَا شِئۡنَا بَدَّلۡنَآ أَمۡثَٰلَهُمۡ تَبۡدِيلًا
Sisi Ndio tuliowaumba na tukalipa uthabiti umbo lao. Na tunapotaka tunawaangamiza na kuwaleta watu walio watiifu zaidi wa Mwenyezi Mungu kuliko wao
Ayah 28إِنَّ هَٰذِهِۦ تَذۡكِرَةࣱۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلࣰ ا
Hakika ndani ya sura hii, kwa yaliyomo ya kuvutia na kuogopesha, ya kuahidi mema na kuonya mabaya, kuna mawaidha kwa viumbe wote. Basi mwenye kujitakia wema nafsi yake ya duniani na Akhera, na ashike njia ya Imani na uchamungu itakayomfikisha kwenye msamaha wa Mwenyezi Mungu na radhi Zake
Ayah 29وَمَا تَشَآءُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمࣰ ا
Na hamtataka jambo lolote miongoni mwa mambo isipokuwa kwa makadirio ya Mwenyezi Mungu na matakwa Yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa hali za viumbe Vyake, ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji na utengezaji Wake
Ayah 30يُدۡخِلُ مَن يَشَآءُ فِي رَحۡمَتِهِۦۚ وَٱلظَّٰلِمِينَ أَعَدَّ لَهُمۡ عَذَابًا أَلِيمَۢا
Anamuingiza Anayemtaka miongoni mwa waja Wake katika rehema Yake na radhi Yake, na wao ni wale walioamini. Na Amewaandalia madhalimu waliokiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu adhabu yenye kuumiza
Ayah 31