Surah Ash-Sharh — The Consolation

Surah Ash-Sharh (The Consolation) — 94/114 · 8 aya. Soma na usikilize kwa maandishi ya Kiarabu na tafsiri ya Kiswahili.

أَلَمۡ نَشۡرَحۡ لَكَ صَدۡرَكَ

Kwani Hatukukunjulia, ewe Mtume, kifua chako kwa sheria za Dini, kulingania watu kwa Mwenyezi Mungu na kujipamba kwa tabia nzuri

Ayah 1

وَوَضَعۡنَا عَنكَ وِزۡرَكَ

Tukakuondolea mazito yako yaliyoemea mgongo wako

Ayah 2

ٱلَّذِيٓ أَنقَضَ ظَهۡرَكَ

na Tukakuweka, kwa matukufu Tuliyokuneemesha

Ayah 3

وَرَفَعۡنَا لَكَ ذِكۡرَكَ

kwenye cheo cha juu

Ayah 4

فَإِنَّ مَعَ ٱلۡعُسۡرِ يُسۡرًا

Usirudi nyuma katika kueneza ujumbe uliotumwa nao kwa makero ya maadui zako. Kwani kwenye dhiki kuna faraji

Ayah 5

إِنَّ مَعَ ٱلۡعُسۡرِ يُسۡرࣰ ا

Hakika kwenye dhiki kuna faraji

Ayah 6

فَإِذَا فَرَغۡتَ فَٱنصَبۡ

Basi utakapomaliza mambo ya kidunia na shughuli zake jipinde kwa kufanya ibada

Ayah 7

وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَٱرۡغَب

Na kwa Mola wako Peke Yake weka matumaini yako

Ayah 8