Surah Al-Humaza — The Traducer
Surah Al-Humaza (The Traducer) — 104/114 · 9 aya. Soma na usikilize kwa maandishi ya Kiarabu na tafsiri ya Kiswahili.
وَيۡلࣱ لِّكُلِّ هُمَزَةࣲ لُّمَزَةٍ
Shari na maangamivu yatampata kila mwenye kusengenya watu na kuwatukana
Ayah 1ٱلَّذِي جَمَعَ مَالࣰ ا وَعَدَّدَهُۥ
Ambaye hamu yake ni kukusanya mali na kuyahesabu
Ayah 2يَحۡسَبُ أَنَّ مَالَهُۥٓ أَخۡلَدَهُۥ
Akidhani kuwa mali yake ambayo ameyakusanya yatampa dhamana ya kuishi milele duniani na kuhepa kuhesabiwa
Ayah 3كَلَّاۖ لَيُنۢبَذَنَّ فِي ٱلۡحُطَمَةِ
Anavyodhania sivyo. Atatiwa ndani ya Moto ambao huvunjavunja kila kinachotiwa
Ayah 4وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡحُطَمَةُ
Lipi lililokujulisha, ewe Mtume, ni upi huo Moto unaovunjavunja
Ayah 5نَارُ ٱللَّهِ ٱلۡمُوقَدَةُ
Huo ni Moto wa Mwenyezi Mungu uliowashwa
Ayah 6ٱلَّتِي تَطَّلِعُ عَلَى ٱلۡأَفۡـِٔدَةِ
Ambao kwa ukali wake hupenyeza miilini ukafikia kwenye nyoyo
Ayah 7إِنَّهَا عَلَيۡهِم مُّؤۡصَدَةࣱ
Moto huo umefungiwa juu yao wakiwa wametiwa minyororo
Ayah 8فِي عَمَدࣲ مُّمَدَّدَةِۭ
na pingu ndefu ili wasitoke
Ayah 9