Surah Al-Falaq — The Dawn

Surah Al-Falaq (The Dawn) — 113/114 · 5 aya. Soma na usikilize kwa maandishi ya Kiarabu na tafsiri ya Kiswahili.

قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلۡفَلَقِ

Sema, ewe Mtume, «Najilinda na kutaka hifadhi kwa Bwana wa asubuhi

Ayah 1

مِن شَرِّ مَا خَلَقَ

«Kutokana na shari la viumbe na udhia wao

Ayah 2

وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ

«Na shari la usiku wenye giza lingi ungiapo na ujikitapo na mashari na maudhi mbalimbali yaliyomo ndani yake

Ayah 3

وَمِن شَرِّ ٱلنَّفَّٰثَٰتِ فِي ٱلۡعُقَدِ

«Na shari la wchawi wenye kupuliza kwenye mafundo wanayoyafunga kwa lengo la kuroga

Ayah 4

وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ

«Na shari la hasidi mwenye kutukia watu, anapowahusudu na kuwadhuru, kwa kutaka neema za Mwenyezi Mungu Aliyewaneemesha ziwaondokee.»

Ayah 5