Surah Al-Kaafiroon — The Disbelievers
Surah Al-Kaafiroon (The Disbelievers) — 109/114 · 6 aya. Soma na usikilize kwa maandishi ya Kiarabu na tafsiri ya Kiswahili.
قُلۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡكَٰفِرُونَ
Sema, ewe Mtume, kuwaambia waliokufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake: «Enyi wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu
Ayah 1لَآ أَعۡبُدُ مَا تَعۡبُدُونَ
«Mimi siabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa urongo
Ayah 2وَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ
«Wala nyinyi si wenye kuabudu Mola Mmoja ninayemuabudu Ambaye ndiye Anayestahiki kuabudiwa
Ayah 3وَلَآ أَنَا۠ عَابِدࣱ مَّا عَبَدتُّمۡ
«Wala mimi si mwenye kuabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa urongo
Ayah 4وَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ
«Wala nyinyi si wenye kuabudu mbeleni ninayemuabudu.» Aya hii imeteremka juu ya watu makhsusi miongoni mwa washirikina ambao Mwenyezi Mungu Alijua kuwa hawataamini kabisa
Ayah 5لَكُمۡ دِينُكُمۡ وَلِيَ دِينِ
«Nyinyi mna dini yenu mnayoiamini na mimi nina Dini yangu ambayo sitaki nyingine.»
Ayah 6