Surah Al-Kawthar — Abundance

Surah Al-Kawthar (Abundance) — 108/114 · 3 aya. Soma na usikilize kwa maandishi ya Kiarabu na tafsiri ya Kiswahili.

إِنَّآ أَعۡطَيۡنَٰكَ ٱلۡكَوۡثَرَ

Sisi tumekupa, ewe Nabii, kheri nyingi za dunia na Akhera, miongoni mwazo ni mto wa Kauthar ulioko Peponi ambao pambizo zake ni mahema ya lulu na mchanga wake ni miski

Ayah 1

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَٱنۡحَرۡ

Basi, mtakasie Mola wako ibada yako yote na uchinje mnyama wako kwa ajili Yake, Peke Yake, pamoja na kutaja jina Lake

Ayah 2

إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ ٱلۡأَبۡتَرُ

Mwenye kukutukia wewe na kuyatukia uliyokuja nayo ya uongofu na nuru ndiye itakayokatika athari yake na yeye mwenyewe kukatiwa kila kheri

Ayah 3