Surah Al-Ghaashiya — The Overwhelming

Surah Al-Ghaashiya (The Overwhelming) — 88/114 · 26 aya. Soma na usikilize kwa maandishi ya Kiarabu na tafsiri ya Kiswahili.

هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلۡغَٰشِيَةِ

Je, ilikujia,ewe Mtume, habari ya Kiyama chenye vituko venye kuwaenea watu

Ayah 1

وُجُوهࣱ يَوۡمَئِذٍ خَٰشِعَةٌ

Nyuso za Makafiri, Siku hiyo, zitakuwa zimenyongeka kwa adhabu

Ayah 2

عَامِلَةࣱ نَّاصِبَةࣱ‏

Zishughulishie, zimechoka na kutaabika

Ayah 3

تَصۡلَىٰ نَارًا حَامِيَةࣰ‏

Zinachomwa kwa Moto wenye kuwaka kwa ukali

Ayah 4

تُسۡقَىٰ مِنۡ عَيۡنٍ ءَانِيَةࣲ‏

Zitanyweshwa maji ya chemchemi yenye moto sana

Ayah 5

لَّيۡسَ لَهُمۡ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعࣲ‏

Watu wa Motoni hawatakuwa na chakula isipokuwa kinachotoka kwenye mti wa miba ilioshikana na chini. Ni kibaya sana chakula hiko na ni kichafu mno

Ayah 6

لَّا يُسۡمِنُ وَلَا يُغۡنِي مِن جُوعࣲ‏

Hakimnoneshi mwenye kukila, awapo amekonda, wala hakimuondolei njaa, awapo na njaa

Ayah 7

وُجُوهࣱ يَوۡمَئِذࣲ نَّاعِمَةࣱ‏

Nyuso za Waumini, siku ya Kiyama, zitakuwa kwenye neema

Ayah 8

لِّسَعۡيِهَا رَاضِيَةࣱ‏

Kwa kuwa zilijishughulisha ulimwenguni kumtii Mwenyezi Mungu na kuridhika na Akhera

Ayah 9

فِي جَنَّةٍ عَالِيَةࣲ‏

Zitakuwa kwenye Pepo ya daraja ya juu

Ayah 10

لَّا تَسۡمَعُ فِيهَا لَٰغِيَةࣰ‏

Hutasikia humo hata neno moja la upuuzi

Ayah 11

فِيهَا عَيۡنࣱ جَارِيَةࣱ‏

Ndani yake kuna chemchemi yenye kuteremka maji yake

Ayah 12

فِيهَا سُرُرࣱ مَّرۡفُوعَةࣱ‏

Ndani yake mna vitanda vilioangatika

Ayah 13

وَأَكۡوَابࣱ مَّوۡضُوعَةࣱ‏

na vikombe vilivyotayarishwa kwa wenye kunywa

Ayah 14

وَنَمَارِقُ مَصۡفُوفَةࣱ‏

na mito iliyopangwa, mmoja baada ya mwingine

Ayah 15

وَزَرَابِيُّ مَبۡثُوثَةٌ

na mazulia mengi yaliyotandikwa

Ayah 16

أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى ٱلۡإِبِلِ كَيۡفَ خُلِقَتۡ

Kwani, hawa makafiri wenye kukanusha, hawaangalii ngamia namna walivyoumbwa kiajabu

Ayah 17

وَإِلَى ٱلسَّمَآءِ كَيۡفَ رُفِعَتۡ

Na mbingu namna zlizoinuliwa juu kwa namna ya kupendeza

Ayah 18

وَإِلَى ٱلۡجِبَالِ كَيۡفَ نُصِبَتۡ

Na milima namna iliyoimarishwa ukapatikana uthabiti na utulivu wa ardhi

Ayah 19

وَإِلَى ٱلۡأَرۡضِ كَيۡفَ سُطِحَتۡ

Na ardhi namna ilivyotandikwa na kutayarishwa

Ayah 20

فَذَكِّرۡ إِنَّمَآ أَنتَ مُذَكِّرࣱ‏

Basi wawaidhie, ewe Mtume, wale wenye kupa nyongo yale uliyotumilizwa kwayo wala usihuzunike kwa kupa mgongo kwao

Ayah 21

لَّسۡتَ عَلَيۡهِم بِمُصَيۡطِرٍ

Kwani wewe ni muwaidhiaji kwao, na si juu yako kuwalazimisha kuamini

Ayah 22

إِلَّا مَن تَوَلَّىٰ وَكَفَرَ

Lakini yule mwenye kuyapa mgongo makumbusho na mawaidha na akawa mkakamavu kwenye ukafiri wake

Ayah 23

فَيُعَذِّبُهُ ٱللَّهُ ٱلۡعَذَابَ ٱلۡأَكۡبَرَ

Mwenyezi Mungu Atamuadhibu adhabu kali Motoni

Ayah 24

إِنَّ إِلَيۡنَآ إِيَابَهُمۡ

Hakika wao watarudi kwetu baada ya kufa

Ayah 25

ثُمَّ إِنَّ عَلَيۡنَا حِسَابَهُم

Kisha ni juu yetu kuwalipa kwa waliyoyafanya

Ayah 26