Surah Al-Maa'un — Almsgiving

Surah Al-Maa'un (Almsgiving) — 107/114 · 7 aya. Soma na usikilize kwa maandishi ya Kiarabu na tafsiri ya Kiswahili.

أَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي يُكَذِّبُ بِٱلدِّينِ

Je, waiona hali ya yule ambaye akanusha kufufuliwa na kulipwa

Ayah 1

فَذَٰلِكَ ٱلَّذِي يَدُعُّ ٱلۡيَتِيمَ

Huyo ndiye yule anayemkaripia yatima kwa nguvu akimnyima haki yake kwa sababu ya ususuavu wa moyo wake

Ayah 2

وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ

Na wala hawahimizi wengine kulisha masikini. Vipi yeye mwenyewe atamlisha

Ayah 3

فَوَيۡلࣱ لِّلۡمُصَلِّينَ

Basi adhabu kali itawafikia wenye kusali

Ayah 4

ٱلَّذِينَ هُمۡ عَن صَلَاتِهِمۡ سَاهُونَ

ambao wameghafilika na Swala zao: hawazisimamishi kama ipasavyo wala hawazisali kwa nyakati zake

Ayah 5

ٱلَّذِينَ هُمۡ يُرَآءُونَ

Ambao huonyesha watu amali zao za kheri kwa njia ya ria

Ayah 6

وَيَمۡنَعُونَ ٱلۡمَاعُونَ

Na wanakataa kuwaazima watu vitu ambavyo hawadhuriki kwa kuviazima, kama vyombo vya kutumia na vinginevyo. Wao hawakujifanyia wema nafsi zao kumuabudu Mola wao wala hawakuwafanyia wema viumbe Vyake

Ayah 7