Surah An-Naas — Mankind
Surah An-Naas (Mankind) — 114/114 · 6 aya. Soma na usikilize kwa maandishi ya Kiarabu na tafsiri ya Kiswahili.
قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلنَّاسِ
Sema, ewe Mtume, «Ninajilinda na kutaka hifadhi kwa Bwana wa watu, Mwenye uweza, Peke Yake, wa kulirudisha shari lao
Ayah 1مَلِكِ ٱلنَّاسِ
«Mfalme wa watu, Mwenye kupeleka mambo yao yote Anavyotaka, Aliye Mkwasi kutowahitajia
Ayah 2إِلَٰهِ ٱلنَّاسِ
«Mola wa watu, Ambaye hapana mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye
Ayah 3مِن شَرِّ ٱلۡوَسۡوَاسِ ٱلۡخَنَّاسِ
«Kutokana na udhia wa shetani ambaye hutia watu wasiwasi wanapoghafilika na hujificha atajwapo Mwenyezi Mungu
Ayah 4ٱلَّذِي يُوَسۡوِسُ فِي صُدُورِ ٱلنَّاسِ
«Mwenye kupenyeza shari na shaka kwenye vifua vya watu
Ayah 5مِنَ ٱلۡجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ
«Miongoni mwa mashetani wa kijini na kibinadamu.»
Ayah 6