Surah Az-Zalzala — The Earthquake

Surah Az-Zalzala (The Earthquake) — 99/114 · 8 aya. Soma na usikilize kwa maandishi ya Kiarabu na tafsiri ya Kiswahili.

إِذَا زُلۡزِلَتِ ٱلۡأَرۡضُ زِلۡزَالَهَا

Itakapotikiswa ardhi mtikiso wa nguvu

Ayah 1

وَأَخۡرَجَتِ ٱلۡأَرۡضُ أَثۡقَالَهَا

Na ikatoa vilivyomo ndani yake: wafu na makandi

Ayah 2

وَقَالَ ٱلۡإِنسَٰنُ مَا لَهَا

Na akauliza binadamu, kwa babaiko, «Imezukiwa na nini?»

Ayah 3

يَوۡمَئِذࣲ تُحَدِّثُ أَخۡبَارَهَا

Siku ya Kiyama ardhi itatoa habari ya mambo iliyofanyiwa ya uzuri na ubaya

Ayah 4

بِأَنَّ رَبَّكَ أَوۡحَىٰ لَهَا

kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Ameiamuru itoe habari ya mambo iliyofanyiwa

Ayah 5

يَوۡمَئِذࣲ يَصۡدُرُ ٱلنَّاسُ أَشۡتَاتࣰ ا لِّيُرَوۡاْ أَعۡمَٰلَهُمۡ

Siku hiyo wataondoka kutoka kwenye kisimamo cha Hesabu wakiwa makundi, ili Mwenyezi Mungu Awaoneshe waliyoyatenda, mazuri na mabaya, na Awalipe kwayo

Ayah 6

فَمَن يَعۡمَلۡ مِثۡقَالَ ذَرَّةٍ خَيۡرࣰ ا يَرَهُۥ

Yoyote mwenye kufanya jema wezani wa chungu mdogo atayaona malipo yake Akhera

Ayah 7

وَمَن يَعۡمَلۡ مِثۡقَالَ ذَرَّةࣲ شَرࣰّ ا يَرَهُۥ

Na yoyote mwenye kufanya baya wezani wa chungu mdogo atayaona malipo yake Akhera

Ayah 8