Surah At-Tur — The Mount

Surah At-Tur (The Mount) — 52/114 · 49 aya. Soma na usikilize kwa maandishi ya Kiarabu na tafsiri ya Kiswahili.

وَٱلطُّورِ

Anaapa Mwenyezi Mungu kwa Ṭūr, nalo ni jabali ambalo juu yake Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Alizungumza na Mūsā

Ayah 1

وَكِتَٰبࣲ مَّسۡطُورࣲ‏

Na kwa Kitabu kilichoandikwa, nacho ni Qur’ani

Ayah 2

فِي رَقࣲّ مَّنشُورࣲ‏

kwenye nyaraka zilizokunjuliwa

Ayah 3

وَٱلۡبَيۡتِ ٱلۡمَعۡمُورِ

Na kwa Nyumba Iliyoamirishwa kwa Malaika watukufu wenye kuizunguka daima

Ayah 4

وَٱلسَّقۡفِ ٱلۡمَرۡفُوعِ

Na kwa sakafu iliyoinuliwa juu, nayo ni uwingu wa duniani

Ayah 5

وَٱلۡبَحۡرِ ٱلۡمَسۡجُورِ

Na kwa bahari iliyowashwa moto, iliyojaa maji

Ayah 6

إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ لَوَٰقِعࣱ‏

Hakika adhabu ya Mola Wako, ewe Mtume, ni yenye kuwashukia makafiri

Ayah 7

مَّا لَهُۥ مِن دَافِعࣲ‏

Hakuna kizuizi cha kuizuia itakaposhuka

Ayah 8

يَوۡمَ تَمُورُ ٱلسَّمَآءُ مَوۡرࣰ ا

Siku ya mbingu kutetemeka mpango wake kuharibika na pande zake kusukikasukika, na hapo ni wakati wa mwisho wa dunia

Ayah 9

وَتَسِيرُ ٱلۡجِبَالُ سَيۡرࣰ ا

na majabali yaondoke mahali pake na yatembee kama vile mawingu yanavyotembea

Ayah 10

فَوَيۡلࣱ يَوۡمَئِذࣲ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Maangamivu katika Siku hii ni yenye kuwashukia wakanushaji

Ayah 11

ٱلَّذِينَ هُمۡ فِي خَوۡضࣲ يَلۡعَبُونَ

Ambao wao wamevama ndani ya ubatilifu wanapumbaa nao na wanaifanya dini yao kuwa ni shere na mchezo

Ayah 12

يَوۡمَ يُدَعُّونَ إِلَىٰ نَارِ جَهَنَّمَ دَعًّا

Siku ya kusukumwa hawa wakanushaji msukumo wa nguvu wenye kuwadhalilisha hadi kwenye Moto wa Jahanamu

Ayah 13

هَٰذِهِ ٱلنَّارُ ٱلَّتِي كُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ

Na waambiwe kwa njia ya kuwalaumu na kuwakaripia, «Huu ndio huo Moto ambao mlikuwa mkiukanusha

Ayah 14

أَفَسِحۡرٌ هَٰذَآ أَمۡ أَنتُمۡ لَا تُبۡصِرُونَ

«Je, ni uchawi adhabu hii mnayoishuhudia au nyinyi hamtazami

Ayah 15

ٱصۡلَوۡهَا فَٱصۡبِرُوٓاْ أَوۡ لَا تَصۡبِرُواْ سَوَآءٌ عَلَيۡكُمۡۖ إِنَّمَا تُجۡزَوۡنَ مَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Onjeni ukali wa Moto huu. Vumilieni uchungu wake na ukali wake au msiyavumilie hayo, hamtahafifishiwa adhabu na hamtatoka humo. Ni sawasawa kwenu nyinyi mkivumilia au mkitovumilia. Hakika nyinyi mnalipwa tu yale mliokuwa mkiyafanya duniani

Ayah 16

إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّٰتࣲ وَنَعِيمࣲ‏

Hakika wachamungu watakuwa kwenye mabustani ya Pepo na neema kubwa

Ayah 17

فَٰكِهِينَ بِمَآ ءَاتَىٰهُمۡ رَبُّهُمۡ وَوَقَىٰهُمۡ رَبُّهُمۡ عَذَابَ ٱلۡجَحِيمِ

Watajistarehesha kwa vile Alivyowapa Mwenyezi Mungu vya neema miongoni mwa aina mbalimbali za ladha na starehe, na Atawaokoa mwenyezi Mungu kutokana na adhabu ya Moto

Ayah 18

كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Kuleni chakula kwa furaha, na mnywe kinywaji chenye ladha, yakiwa ni malipo ya matendo mema mliyoyafanya duniani

Ayah 19

مُتَّكِـِٔينَ عَلَىٰ سُرُرࣲ مَّصۡفُوفَةࣲۖ وَزَوَّجۡنَٰهُم بِحُورٍ عِينࣲ‏

Na wao watakuwa wametegemea, wako juu ya vitanda vinavyoelekeana, na tutawaoza wanawake weupe wenye macho mapana yaliyo mazuri

Ayah 20

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَٱتَّبَعَتۡهُمۡ ذُرِّيَّتُهُم بِإِيمَٰنٍ أَلۡحَقۡنَا بِهِمۡ ذُرِّيَّتَهُمۡ وَمَآ أَلَتۡنَٰهُم مِّنۡ عَمَلِهِم مِّن شَيۡءࣲۚ كُلُّ ٱمۡرِيِٕۭ بِمَا كَسَبَ رَهِينࣱ‏

Na wale walioamini na wakafuatwa na watoto wao katika hiyo Imani, Tutawakutanisha watoto wao nao katika daraja yao Peponi, hata kama hawakufikia matendo ya wazazi wao, ili wazazi wafurahike na watoto wao pamoja na wao katika daraja zao. Watakusanywa baina yao kwenye hali nzuri zaidi, na hatutawapunguzia chochote katika matendo yao mema. Kila mtu anafungwa na matendo yake aliyoyachuma, hatobeba dhambi za watu wengine

Ayah 21

وَأَمۡدَدۡنَٰهُم بِفَٰكِهَةࣲ وَلَحۡمࣲ مِّمَّا يَشۡتَهُونَ

Na tutawaongezea, juu ya starehe hizo zilizotajwa, matunda na nyama miongoni mwa vitu vinavyopendwa na kutamaniwa

Ayah 22

يَتَنَٰزَعُونَ فِيهَا كَأۡسࣰ ا لَّا لَغۡوࣱ فِيهَا وَلَا تَأۡثِيمࣱ‏

Na miongoni mwa starehe hizo ni kuwa wao watapeana gilasi ya pombe, mmoja wao atampa mwenzake, ili furaha yao ikamilike. Kinywaji hiki kinatafautiana na pombe ya duniani, hakimleweshi akili mwenye kukinywa, wala hakisababishi kubobokwa, wala maneno ya makosa na maasia

Ayah 23

۞وَيَطُوفُ عَلَيۡهِمۡ غِلۡمَانࣱ لَّهُمۡ كَأَنَّهُمۡ لُؤۡلُؤࣱ مَّكۡنُونࣱ‏

Na watawazunguka watumishi waliotayarishwa kuwatumikia kama kwamba wao katika usafi na weupe na utungaji nidhamu ni lulu iliyohifadhiwa kwenye mashaza yake

Ayah 24

وَأَقۡبَلَ بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضࣲ يَتَسَآءَلُونَ

Watageukiana watu wa Peponi kuulizana wao kwa wao juu ya ukubwa wa yale waliyonayo na sababu ya kuyapata

Ayah 25

قَالُوٓاْ إِنَّا كُنَّا قَبۡلُ فِيٓ أَهۡلِنَا مُشۡفِقِينَ

Watasema, «Sisi tulikuwa kabla, huko duniani, na sisi tuko baina ya watu wetu, tunamuogopa Mola wetu, tuna hadhari na adhabu Yake na mateso yake Siku ya Kiyama

Ayah 26

فَمَنَّ ٱللَّهُ عَلَيۡنَا وَوَقَىٰنَا عَذَابَ ٱلسَّمُومِ

Mwenyezi Mungu Akatuneemesha kwa uongofu na taufiki na Akatuokoa na adhabu ya vuke la Jahanamu, nalo ni moto wake na joto lake. Sisi tulikuwa, hapo kabla, tukimnyenyekea Yeye Peke Yake, hatumshirikishi na Yeye yoyote asiyekuwa Yeye, Atulinde na adhabu ya vuke la Motoni na Atupeleke kwenye starehe ya Peponi

Ayah 27

إِنَّا كُنَّا مِن قَبۡلُ نَدۡعُوهُۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡبَرُّ ٱلرَّحِيمُ

Mwenyezi Mungu Akatukubalia maombi yetu, na Akatupa tulichokiomba. Hakika Yeye Ndiye Mwingi wa kheri, Mwenye kurehemu. Na miongoni mwa wingi wa kheri Zake na rehema Zake kwetu ni kule kutupa radhi zake na Pepo, na kutuepusha na hasira Zake na Moto.»

Ayah 28

فَذَكِّرۡ فَمَآ أَنتَ بِنِعۡمَتِ رَبِّكَ بِكَاهِنࣲ وَلَا مَجۡنُونٍ

Basi wawaidhie, ewe Mtume, wale uliotumilizwa kwao kwa Qur’ani, kwani hukuwa wewe, kwa neema ya Mwenyezi Mungu Aliokuneemesha kwayo ya unabii na busara ya akili, ni kuhani anayetoa habari za ghaibu bila ujuzi wala mwendawazimu asiyejua analolisema, kama wanavyodai

Ayah 29

أَمۡ يَقُولُونَ شَاعِرࣱ نَّتَرَبَّصُ بِهِۦ رَيۡبَ ٱلۡمَنُونِ

Au wanakwambia hao washirikina, ewe Mtume, «Yeye ni mshairi, tunangojea ashukiwe na mauti»

Ayah 30

قُلۡ تَرَبَّصُواْ فَإِنِّي مَعَكُم مِّنَ ٱلۡمُتَرَبِّصِينَ

Waambie, «Yangojeeni mauti yangu, kwani mimi pamoja na nyinyi ni katika wenye kuingojea adhabu yenu, na mtaona ni nani atakayekuwa na mwisho mwema

Ayah 31

أَمۡ تَأۡمُرُهُمۡ أَحۡلَٰمُهُم بِهَٰذَآۚ أَمۡ هُمۡ قَوۡمࣱ طَاغُونَ

Au zinawaamuru akili zao, hao wakanushaji, ziseme neno hili linalogongana (kuwa sifa ya ukuhani, utungaji mashairi, na wendawazimu haiwezekani kukutana wakati mmoja)? Bali wao ni watu waliruka mipaka katika uasi

Ayah 32

أَمۡ يَقُولُونَ تَقَوَّلَهُۥۚ بَل لَّا يُؤۡمِنُونَ

Au wanasema hawa washirikina, «Muhammad Ameibuni Qur’ani yeye mwenyewe?» bali wao hawaamini. Na lau wangaliamini, hawangalilisema walilolisema

Ayah 33

فَلۡيَأۡتُواْ بِحَدِيثࣲ مِّثۡلِهِۦٓ إِن كَانُواْ صَٰدِقِينَ

Basi na walete maneno mfano wa Qur’ani iwapo wao ni wakweli katika madai yao kuwa Muhammad Ameibuni

Ayah 34

أَمۡ خُلِقُواْ مِنۡ غَيۡرِ شَيۡءٍ أَمۡ هُمُ ٱلۡخَٰلِقُونَ

Je, wameumbwa hawa washirikina bila kuwako mwenye kuwaumba na kuwapatisha au wao wamejiumba wenyewe? Na yote mambo mawili haya yametanguka na hayawezekani. Na kwa hivyo, inalazimika kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyewaumba, na Yeye Peke Yake Ndiye Ambaye hakuna anayepasa kuabudiwa, wala kufaa kuabudiwa, isispokuwa Yeye

Ayah 35

أَمۡ خَلَقُواْ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَۚ بَل لَّا يُوقِنُونَ

Au wao wameumba mbingu na ardhi kwa utengezaji huu wa kipekee? Bali wao hawaamini adhabu ya Mwenyezi Mungu, kwa kuwa wao ni washirikina

Ayah 36

أَمۡ عِندَهُمۡ خَزَآئِنُ رَبِّكَ أَمۡ هُمُ ٱلۡمُصَۜيۡطِرُونَ

Au wanazo wao hazina za Mola wako wanazitumia? Au wao ni majebari wanaowagandamiza viumbe vya Mwenyezi Mungu kwa kuwatendesha nguvu na kuwanyanyasa? Mambo si hivyo, bali wao ndio walemevu walio madhaifu

Ayah 37

أَمۡ لَهُمۡ سُلَّمࣱ يَسۡتَمِعُونَ فِيهِۖ فَلۡيَأۡتِ مُسۡتَمِعُهُم بِسُلۡطَٰنࣲ مُّبِينٍ

Au wao wana ngazi ya kupandia mbinguni wanasikiliza huko wahyi kwamba yale waliyonayo ndio haki? Basi na aje, yule anayedai kuwa amesikia hilo, na hoja ya waziwazi yenye kusadikisha madai yake

Ayah 38

أَمۡ لَهُ ٱلۡبَنَٰتُ وَلَكُمُ ٱلۡبَنُونَ

Je, mwenyezi Mungu , aliyetakasika, Ana watoto wa kike na nyinyi mna watoto wa kiume kama mnavyodai kwa uzushi na urongo

Ayah 39

أَمۡ تَسۡـَٔلُهُمۡ أَجۡرࣰ ا فَهُم مِّن مَّغۡرَمࣲ مُّثۡقَلُونَ

Au je unawataka, ewe Mtume, hawa washirikina wakupatie malipo ya kuwafikishia Ujumbe, wakawa wao wana tabu na dhiki ya kujilazimisha malipo unayoyataka kutoka kwao

Ayah 40

أَمۡ عِندَهُمُ ٱلۡغَيۡبُ فَهُمۡ يَكۡتُبُونَ

Au je wao wana ujuzi wa ghaibu wakawa wanawaandikia watu na kuwapa habari yake? Mambo si hivyo, kwani hakika ya mambo ni kwamba hakuna anayejua ghaibu iliyo mbinguni na ardhini isipokuwa Mwenyezi Mungu

Ayah 41

أَمۡ يُرِيدُونَ كَيۡدࣰ اۖ فَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ هُمُ ٱلۡمَكِيدُونَ

Bali wao wanataka kumfanyia vitimbi Mtume wa Mwenyezi Mungu na Waumini. Basi hao makafiri, vitimbi vyao na njama zao vitawarudia wao wenyewe

Ayah 42

أَمۡ لَهُمۡ إِلَٰهٌ غَيۡرُ ٱللَّهِۚ سُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Au wao wana muabudiwa anayestahiki kuabudiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu? Ametakasika Mwenyezi Mungu na kutukuka na yale wanayoshirikisha. Kwani Yeye Hana mshirika katika mamlaka, na Hana mshirika katika Upweke na ustahiki wa kuabudiwa

Ayah 43

وَإِن يَرَوۡاْ كِسۡفࣰ ا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ سَاقِطࣰ ا يَقُولُواْ سَحَابࣱ مَّرۡكُومࣱ‏

Na wakikiona hawa washirikina kipande cha mbingu kinawaangukia, kikiwa ni adhabu kwao, hawataacha yale waliyo nayo ya ukanushaji, na watasema, «Haya ni mawingu yamekusanyika na kupandana.»

Ayah 44

فَذَرۡهُمۡ حَتَّىٰ يُلَٰقُواْ يَوۡمَهُمُ ٱلَّذِي فِيهِ يُصۡعَقُونَ

Basi waache, ewe Mtume, hawa washirikina mpaka wakutane na Siku yao hiyo ya wao kuangamizwa, nayo ni Siku ya Kiyama

Ayah 45

يَوۡمَ لَا يُغۡنِي عَنۡهُمۡ كَيۡدُهُمۡ شَيۡـࣰٔ ا وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ

Katika Siku hiyo havitawazuilia wao vitimbi vyao kotokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu kitu chochote, na hatawanusuru yoyote kuwaokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu

Ayah 46

وَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُواْ عَذَابࣰ ا دُونَ ذَٰلِكَ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ

Hakika madhalimu hawa watakuta adhabu duniani, kabla ya adhabu ya Siku ya Kiyama, ya kuuawa, kukamatwa mateka, adhabu ya kaburini na nyinginezo. Lakini wengi wa watu hawajui hilo

Ayah 47

وَٱصۡبِرۡ لِحُكۡمِ رَبِّكَ فَإِنَّكَ بِأَعۡيُنِنَاۖ وَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ حِينَ تَقُومُ

Na uivumilie, ewe Mtume, hukumu ya Mola wako na amri Yake juu ujumbe Aliyokubebesha na juu ya makero yanayokupata kutoka kwa watu wako, hakika wewe uko kwenye maangalizi yetu, hifadhi na utunzi. Na umtakase Mola Wako kwa kumsifu unaposimama kuswali na unapoinuka kutoka usingizini

Ayah 48

وَمِنَ ٱلَّيۡلِ فَسَبِّحۡهُ وَإِدۡبَٰرَ ٱلنُّجُومِ

Na kwenye kipindi cha usiku mtakase Mola wako kwa kumsifu, umtukuze na umswalie. Na ufanye hayo kwenye kipindi cha Swala ya Asubuhi wakati wa nyota kuondoka. Katika aya hizi pana kuthibitisha sifa ya macho mawili kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa inavyonasibiana na Yeye, bila kufananisha na viumbe Vyake au kuieleza dhati Yake vile ilivyo, kutakasika na kila sifa ya upungufu ni Kwake na sifa njema zote ni Zake, kama lilivyothibiti hilo katika Sunnah na kukubaliana juu yake wanavyuoni waliopita wa Ummah huu

Ayah 49