Surah Al-Hijr — The Rock

Surah Al-Hijr (The Rock) — 15/114 · 99 aya. Soma na usikilize kwa maandishi ya Kiarabu na tafsiri ya Kiswahili.

الٓرۚ تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِ وَقُرۡءَانࣲ مُّبِينࣲ‏

(Alif, Lām, Rā) Yametangulia maelezo kuhusu herufi zilizokatwa na kutengwa. Hizo ni aya tukufu miongoni mwa aya za Kitabu kitukufu kilichoteremshwa kwa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye. Nazo ni aya za Qur’ani zenye kufafanua kweli kwa matamko mazuri zaidi na yaliyo wazi zaidi na yenye kuonyesha zaidi makusudio. Kitabu na Qur’ani ni kitu kimoja ; na hapa Mwenyezi Mungu Ameyakusanya pamoja majina mawili

Ayah 1

رُّبَمَا يَوَدُّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَوۡ كَانُواْ مُسۡلِمِينَ

Makafiri watatamani, watakapowaona Waumini walioasi wakitoka Motoni, lau wao walikuwa ni wenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu wakawa ni wenye kutoka kama wao

Ayah 2

ذَرۡهُمۡ يَأۡكُلُواْ وَيَتَمَتَّعُواْ وَيُلۡهِهِمُ ٱلۡأَمَلُۖ فَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ

Waache, ewe Mtume, hao makafiri wapate kula na wastarehe na ulimwengu wao na iwashughulishe tamaa ya huo ulimwengu wasimtii Mwenyezi Mungu, watakuja kujua mwisho wa mambo yao ambayo ni hasara ya duniani na Akhera

Ayah 3

وَمَآ أَهۡلَكۡنَا مِن قَرۡيَةٍ إِلَّا وَلَهَا كِتَابࣱ مَّعۡلُومࣱ‏

Na wakiomba kuteremshiwa adhabu, kwa kukukanusha, ewe Mtume, basi sisi hatuuangamizi mji, isipokuwa uwapo wakati wa kuangamizwa umeshapangwa; hatutawaangamiza mpaka waufikie mfano wa wale waliowatangulia

Ayah 4

مَّا تَسۡبِقُ مِنۡ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا يَسۡتَـٔۡخِرُونَ

Hakuna watu wowote watakaoupita muda wao uliowekwa wakauzidisha wala kuutangulia wakaupunguza

Ayah 5

وَقَالُواْ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِي نُزِّلَ عَلَيۡهِ ٱلذِّكۡرُ إِنَّكَ لَمَجۡنُونࣱ‏

Na wenye kumkanusha Muhammad, rehema na amani zimshukie, walisema kwa njia ya shere, «Ewe yule ulioteremshiwa Qur’ani, ‘wewe umerukwa na akili.’

Ayah 6

لَّوۡمَا تَأۡتِينَا بِٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ

Si utuletee Malaika iwapo wewe ni mkweli wapate kutoa ushahidi kwamba Mwenyezi Mungu Amekutumiliza.»

Ayah 7

مَا نُنَزِّلُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ إِلَّا بِٱلۡحَقِّ وَمَا كَانُوٓاْ إِذࣰ ا مُّنظَرِينَ

Na Mwenyezi Mungu Akawajibu: Sisi hatuwateremshi Malaika isipokuwa kwa adhabu ambayo haina kucheleweshwa kwa asiyeamini na hawakuwa ni wenye kuachwa wakati Malaika watakapoteremka

Ayah 8

إِنَّا نَحۡنُ نَزَّلۡنَا ٱلذِّكۡرَ وَإِنَّا لَهُۥ لَحَٰفِظُونَ

Hakika sisi tumeiteremsha Qur’ani kwa Nabii Muhammad, rehema na amani zimshukiye, na hakika sisi tunachukua ahadi kuitunza isiongezwe, isipunguzwe wala sehemu yoyote katika hiyo isipotee

Ayah 9

وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ فِي شِيَعِ ٱلۡأَوَّلِينَ

Na kwa hakika tulitumiliza kabla yako, ewe Mtume, Wajumbe kati ya makundi ya wa mwanzo

Ayah 10

وَمَا يَأۡتِيهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ

Hakuna Mjumbe yoyote aliwajia wao isipokuwa walikuwa wakimfanyia shere.Katika haya pana kumliwaza Mtume, rehema na amani zimshukie. Na kama walivyokufanyia hawa, hivyo ndivyo walivyofanyiwa Mitume kabla yako

Ayah 11

كَذَٰلِكَ نَسۡلُكُهُۥ فِي قُلُوبِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ

Kama tulivyoutia ukafiri kwenye nyoyo za ummah waliotangulia kwa sababu ya kuwafanyia shere Mitume na kuwakanusha, hivyo ndivyo tunavyofanya kwenye nyoyo za washirikina miongoni mwa watu wako waliofanya uhalifu wa kumkanusha Mwenyezi Mungu na kuwakanusha Mitume Wake

Ayah 12

لَا يُؤۡمِنُونَ بِهِۦ وَقَدۡ خَلَتۡ سُنَّةُ ٱلۡأَوَّلِينَ

hawauamini Ukumbusho ulioteremshwa kwako. Na umeshapita mwendo wa wamwanzo wa kuwaangamiza wakanushaji. Na hawa ni kama wao, wataangamizwa wenye kuendelea na ukafiri na ukanushaji miongoni mwao

Ayah 13

وَلَوۡ فَتَحۡنَا عَلَيۡهِم بَابࣰ ا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ فَظَلُّواْ فِيهِ يَعۡرُجُونَ

Na lau tuliwafungulia makafiri wa Makkah mlango wa mbingu, wakaendelea kupanda kuingia ndani wapate kuyashuhudia yaliyomo mbinguni ya ajabau za ufalme wa Mwenyezi Mungu, hawangaliamini

Ayah 14

لَقَالُوٓاْ إِنَّمَا سُكِّرَتۡ أَبۡصَٰرُنَا بَلۡ نَحۡنُ قَوۡمࣱ مَّسۡحُورُونَ

na wangalisema, «Macho yetu yamerogwa mpaka tumekuwa tunaona tusiyoyaona. Sisi tumerogwa tu na Muhammad kwenye akili zetu.»

Ayah 15

وَلَقَدۡ جَعَلۡنَا فِي ٱلسَّمَآءِ بُرُوجࣰ ا وَزَيَّنَّٰهَا لِلنَّٰظِرِينَ

Na miongoni mwa dalili za uweza wetu ni kwamba sisi tumeweka kwenye uwingu wa karibu vituo ya sayari kushukia, ambayo kwayo zinajulikana njia, nyakati, urutuba na ukavu, na tumeupamba uwingu huu kwa nyota ili wenye kuziangalia wataamali na wazingatie

Ayah 16

وَحَفِظۡنَٰهَا مِن كُلِّ شَيۡطَٰنࣲ رَّجِيمٍ

Na tumeuhifadhi uwingu huo na kila Shetani Aliyetolewa na aliyefukuzwa kutoka kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu ili asiufikie

Ayah 17

إِلَّا مَنِ ٱسۡتَرَقَ ٱلسَّمۡعَ فَأَتۡبَعَهُۥ شِهَابࣱ مُّبِينࣱ‏

Isipokuwa aliyetega sikio kusikiliza maneno ya watu wa juu baadhi ya nyakati, akafikiwa na sayari inayotoa mwangaza na kumchoma.Na huenda Shetani akamddokeza rafiki yake baadhi ya habari alizozisikia kwa kutegea kabla hajateketezwa na kimondo

Ayah 18

وَٱلۡأَرۡضَ مَدَدۡنَٰهَا وَأَلۡقَيۡنَا فِيهَا رَوَٰسِيَ وَأَنۢبَتۡنَا فِيهَا مِن كُلِّ شَيۡءࣲ مَّوۡزُونࣲ‏

Na ardhi tumeinyosha ikawa kunjufu, tukaweka juu yake majabali yenye kuiimarisha , tuakaotesha kila aina ya mimea ambayo waja wanaihitajia kwa kipimo kinachojulikana

Ayah 19

وَجَعَلۡنَا لَكُمۡ فِيهَا مَعَٰيِشَ وَمَن لَّسۡتُمۡ لَهُۥ بِرَٰزِقِينَ

Na tukawawekea nyinyi humo vitu mnavyovihitajia katika maisha yenu miongoni mwa makulima, wanyama, aina mbalimbali ya shughuli za kujipatia maisha na vinginevyo. Na tukawaumbia nyinyi watoto, watumishi na wanyama manaonufaika nao. Na riziki zao haziko juu yenu, bali ziko juu ya Mwenyezi Mungu Bwana wa viumbe vyote kwa wema utokao Kwake na ukarimu

Ayah 20

وَإِن مِّن شَيۡءٍ إِلَّا عِندَنَا خَزَآئِنُهُۥ وَمَا نُنَزِّلُهُۥٓ إِلَّا بِقَدَرࣲ مَّعۡلُومࣲ‏

Na hakuna chochote cha manufaa ya waja isipokuwa ziko kwetu hazina zake za kila aina, na hatukiteremshi isipokuwa kwa kadiri iliyowekewa mpaka, kama vile tutakavyo. Hazina zote ziko mkononi mwa Mwenyezi Mungu, Anampa Anayemtaka na Anamzuilia Anayemtaka, kulingana na rehema Yake kunjufu na hekima Yake kubwa

Ayah 21

وَأَرۡسَلۡنَا ٱلرِّيَٰحَ لَوَٰقِحَ فَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءࣰ فَأَسۡقَيۡنَٰكُمُوهُ وَمَآ أَنتُمۡ لَهُۥ بِخَٰزِنِينَ

Na tunatuma upepo na tunaufanya uwe mtiifu kwetu uyajaze mawingu yabubujishe maji na yanyeshe na yanywesheze miti, hapo majani yake yafunguke na mafumba yake yajitokeze. Na mvua inabeba heri na nafuu na tunayateremsha maji yake tuliyowatayarishia nyinyi kwa ajili ya kunywa kwenu, ardhi yenu na wanayama wenu. Na nyinyi si waweza wa kuyahifadhi na kuyaweka akiba, lakini sisi tunawahifadhia kwa kuwahurumia na kuwafanyia hisani

Ayah 22

وَإِنَّا لَنَحۡنُ نُحۡيِۦ وَنُمِيتُ وَنَحۡنُ ٱلۡوَٰرِثُونَ

Ndio sisi tunaompa uhai aliyekufa kwa kumpatisha kutoka kwenye hali ya kutokuwako, na tunamfisha aliyekuwa hai baada ya ajali yake kukoma. Na sisi ndio wenye kuirithi ardhi na walioko juu yake

Ayah 23

وَلَقَدۡ عَلِمۡنَا ٱلۡمُسۡتَقۡدِمِينَ مِنكُمۡ وَلَقَدۡ عَلِمۡنَا ٱلۡمُسۡتَـٔۡخِرِينَ

Kwa hakika tunawajua walioangamia miongoni mwenu tangu Ādam, walio hai na watakaokuja mpaka Siku ya Kiyama

Ayah 24

وَإِنَّ رَبَّكَ هُوَ يَحۡشُرُهُمۡۚ إِنَّهُۥ حَكِيمٌ عَلِيمࣱ‏

Na hakika Mola wako Ndiye Atakayewakusanya wao wahesabiwe na walipwe. Hakika Yeye ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji Wake mambo, ni Mwingi wa ujuzi, hakuna kinachofichika Kwake

Ayah 25

وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ مِن صَلۡصَٰلࣲ مِّنۡ حَمَإࣲ مَّسۡنُونࣲ‏

Kwa hakika tulimuumba Ādam kwa udongo mkavu, ukigongwa unasikiwa sauti. Na udongo huu mkavu ni miongoni mwa udongo mweusi uliogeuka rangi yake na harufu yake kwa kipindi kirefu cha kukaa kwake

Ayah 26

وَٱلۡجَآنَّ خَلَقۡنَٰهُ مِن قَبۡلُ مِن نَّارِ ٱلسَّمُومِ

Na tulimuumba baba wa majini, naye ni Iblisi, kabla ya kuumbwa Ādam, kwa moto mkali sana, usio na moshi

Ayah 27

وَإِذۡ قَالَ رَبُّكَ لِلۡمَلَٰٓئِكَةِ إِنِّي خَٰلِقُۢ بَشَرࣰ ا مِّن صَلۡصَٰلࣲ مِّنۡ حَمَإࣲ مَّسۡنُونࣲ‏

Kumbuka, ewe Mtume, pindi Mola wako Aliposema kuwaambia Malaika, «Mimi nitamuumba mtu kutokana na udongo mkavu. Na udongo huu mkavu unatokana na udongo mweusi uliogeuka rangi

Ayah 28

فَإِذَا سَوَّيۡتُهُۥ وَنَفَخۡتُ فِيهِ مِن رُّوحِي فَقَعُواْ لَهُۥ سَٰجِدِينَ

«Basi nitakapomtengeneza na kulikamilisha umbo lake na nikapuliza roho ndani yake, mwangukieni hali ya kusujudu,» sijida ya maamkizi na heshima na si sijida ya ibada

Ayah 29

فَسَجَدَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ كُلُّهُمۡ أَجۡمَعُونَ

Na Malaika wote walisujudu kwa umoja wao, kama Alivyowaamrisha Mola Wao.. Hakuna yoyote kati yao aliyekataa

Ayah 30

إِلَّآ إِبۡلِيسَ أَبَىٰٓ أَن يَكُونَ مَعَ ٱلسَّٰجِدِينَ

Lakini Iblisi alikataa kumsujudia Ādam pamoja na Malaika waliosujudu

Ayah 31

قَالَ يَٰٓإِبۡلِيسُ مَا لَكَ أَلَّا تَكُونَ مَعَ ٱلسَّٰجِدِينَ

Mwenyezi Mungu Akasema kumwambia Iblisi, «Una nini wewe kutosujudu pamoja na Malaika?»

Ayah 32

قَالَ لَمۡ أَكُن لِّأَسۡجُدَ لِبَشَرٍ خَلَقۡتَهُۥ مِن صَلۡصَٰلࣲ مِّنۡ حَمَإࣲ مَّسۡنُونࣲ‏

Iblisi akasema akionyesha kiburi chake na uhasidi wake, «Hainasibiani na mimi nimsujudie mtu uliyempatisha kutokana na udongo mkavu, uliokuwa mweusi na uliogeuka.»

Ayah 33

قَالَ فَٱخۡرُجۡ مِنۡهَا فَإِنَّكَ رَجِيمࣱ‏

Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Akamwambia, «Basi toka Peponi, wewe ushafukuzwa na umeepushwa na kila jema

Ayah 34

وَإِنَّ عَلَيۡكَ ٱللَّعۡنَةَ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلدِّينِ

umeshukiwa na laana na umewekwa mbali na rehema yangu mpaka Siku ya kufufuliwa watu ili wahesabiwe na walipwe..»

Ayah 35

قَالَ رَبِّ فَأَنظِرۡنِيٓ إِلَىٰ يَوۡمِ يُبۡعَثُونَ

Iblisi akasema, «Ewe Mola wangu! Nipatie muda mpaka siku ya wewe kuwafufua waja wako , nayo ni Siku ya Kiyama.»

Ayah 36

قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ ٱلۡمُنظَرِينَ

Mwenyezi Mungu Akamwambia, «Wewe ni miongoni mwa wale niliowapa muda na kuchelewesha kuwaangamiza mpaka siku ambayo viumbe wote watakufa baada ya Mpulizo wa kwanza

Ayah 37

إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡوَقۡتِ ٱلۡمَعۡلُومِ

na siyo mpaka siku ya Ufufuzi. Na alikubaliwa hilo kwa njia ya kulegezewa na kuachiliwa, na ni mtihani kwa binadamu na majini

Ayah 38

قَالَ رَبِّ بِمَآ أَغۡوَيۡتَنِي لَأُزَيِّنَنَّ لَهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَأُغۡوِيَنَّهُمۡ أَجۡمَعِينَ

Akasema Iblisi, «Mola wangu, kwa sababu ya vile ulivyonipoteza na kunipotosha nitawapambia vizazi vya Ādam kukuasi katika ardhi na nitawapoteza wote wasiione njia ya uongofu

Ayah 39

إِلَّا عِبَادَكَ مِنۡهُمُ ٱلۡمُخۡلَصِينَ

isipokuwa waja wako ambao umewaongoa wakakutakasia ibada peke yako pasi na viumbe wako wengine.»

Ayah 40

قَالَ هَٰذَا صِرَٰطٌ عَلَيَّ مُسۡتَقِيمٌ

Akasema Mwenyezi Mungu , «Hii ni njia nyofu iliyolingana inayofikisha kwangu na kwenye Nyumba ya ukarimu wangu

Ayah 41

إِنَّ عِبَادِي لَيۡسَ لَكَ عَلَيۡهِمۡ سُلۡطَٰنٌ إِلَّا مَنِ ٱتَّبَعَكَ مِنَ ٱلۡغَاوِينَ

Kwa kweli, wale waja wangu ambao wamenitakasia mimi sitakupatia uwezo juu ya nyoyo zao ili uwapoteze kwa uwezo huo na njia iliyonyoka. Lakini uwezo wako utakuwa ni juu ya yule aliyekuandama miongoni mwa wapotofu washirikina ambao wameukubali usimamizi wako na kukutii badala ya kunitii mimi.»

Ayah 42

وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوۡعِدُهُمۡ أَجۡمَعِينَ

Hakika Moto mkali ndio agizo la Iblisi na wafuasi wake wote

Ayah 43

لَهَا سَبۡعَةُ أَبۡوَٰبࣲ لِّكُلِّ بَابࣲ مِّنۡهُمۡ جُزۡءࣱ مَّقۡسُومٌ

Una milango saba , kila mlango uko chini ya mwengine. Kila mlango utakuwa na fungu na sehemu la wafuasi wa Iblisi kulingana na matendo yao

Ayah 44

إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّٰتࣲ وَعُيُونٍ

Hakika wale waliomcha Mwenyezi Mungu, kwa kuyafuata Aliyoyaamrisha na kujiepusha na aliyoyakataza.watakuwa kwenye mabustani ya Pepo na mito ipitayo

Ayah 45

ٱدۡخُلُوهَا بِسَلَٰمٍ ءَامِنِينَ

Wataambiwa, «Ingieni Mabustani haya mkiwa watulivu mumesalimika na kila ovu mumeaminika na kila adhabu

Ayah 46

وَنَزَعۡنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنۡ غِلٍّ إِخۡوَٰنًا عَلَىٰ سُرُرࣲ مُّتَقَٰبِلِينَ

Na tutawaondolea yaliyomo ndani ya nyoyo zao ya chuki na uadui, wataishi Peponi wakiwa ndugu wapendanao, watakaa kwenye vitanda vikubwa na nyuso zao zitaelekeana katika hali ya kuungana na kupendana

Ayah 47

لَا يَمَسُّهُمۡ فِيهَا نَصَبࣱ وَمَا هُم مِّنۡهَا بِمُخۡرَجِينَ

Haitawapata humo tabu wala uchovu. Na wao ni wenye kusalia humo milele

Ayah 48

۞نَبِّئۡ عِبَادِيٓ أَنِّيٓ أَنَا ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ

Wapashe habari, ewe Mtume, waja wangu kwamba mimi ni mwenye kuwasamehe Waumini wenye kutubia, ni mwenye huruma kwao

Ayah 49

وَأَنَّ عَذَابِي هُوَ ٱلۡعَذَابُ ٱلۡأَلِيمُ

na kwamba adhabu yangu ndiyo adhabu iumizayo yenye kutia uchungu kwa wasiotubia

Ayah 50

وَنَبِّئۡهُمۡ عَن ضَيۡفِ إِبۡرَٰهِيمَ

Na wapashe habari, ewe Mtume, kuhusu wageni wa Ibrāhīm miongoni mwa Malaika ambao walimpa habari njema za kupata mwana na za kuangamia kwa jamaa za Lūṭ

Ayah 51

إِذۡ دَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَقَالُواْ سَلَٰمࣰ ا قَالَ إِنَّا مِنكُمۡ وَجِلُونَ

Pindi walipoingia kwake na wakamwamkia kwa kusema, «Amani.» Hapo naye akawarudishia maamkizi ya amani. Kisha akwaletea chakula na wao wasikile, na hapo akasema, «Sisi ni wenye kicho na nyinyi.»

Ayah 52

قَالُواْ لَا تَوۡجَلۡ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَٰمٍ عَلِيمࣲ‏

Malaika wakamwambia, «Usiwe na kicho. Sisi tumekuja kukupa habari njema kwamba utapata mwana atakayekuwa na ujuzi mwingi wa Dini, naye ni Is’ḥāq.»

Ayah 53

قَالَ أَبَشَّرۡتُمُونِي عَلَىٰٓ أَن مَّسَّنِيَ ٱلۡكِبَرُ فَبِمَ تُبَشِّرُونَ

Ibrāhīm akasema, huku yuwaona ajabu, «Mnanipa habari njema za kupata mwana na mimi nishakuwa mtu mzima, na mke wangu pia, ni kwa njia gani mnanipa habari njema hizo za kushangaza?»

Ayah 54

قَالُواْ بَشَّرۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ فَلَا تَكُن مِّنَ ٱلۡقَٰنِطِينَ

Wakasema, «Tunakupa habari njema kwa kweli ambayo Mwenyezi Mungu Ametujulisha nayo. Basi usiwe miongoni mwa waliokata tamaa ya wewe kupata mwana.»

Ayah 55

قَالَ وَمَن يَقۡنَطُ مِن رَّحۡمَةِ رَبِّهِۦٓ إِلَّا ٱلضَّآلُّونَ

Ibrāhīm akasema, «Hakika hawakati tamaa na rehema za Mola wao isipokuwa walio na makosa waliojitenga na njia ya haki.»

Ayah 56

قَالَ فَمَا خَطۡبُكُمۡ أَيُّهَا ٱلۡمُرۡسَلُونَ

Na akasema, «Ni jambo gani kubwa mlilolijia, enyi mliotumwa, kutoka kwa Mwenyezi Mungu?»

Ayah 57

قَالُوٓاْ إِنَّآ أُرۡسِلۡنَآ إِلَىٰ قَوۡمࣲ مُّجۡرِمِينَ

Wakasema, «Hakika Mwenyezi Mungu Ametutuma kuwaangamiza watu wa Lūṭ walio washirikina wapotofu

Ayah 58

إِلَّآ ءَالَ لُوطٍ إِنَّا لَمُنَجُّوهُمۡ أَجۡمَعِينَ

isipokuwa Lūṭ na watu wake waliomuamini, hao hatutawaangamiza na tutawaokoa wote

Ayah 59

إِلَّا ٱمۡرَأَتَهُۥ قَدَّرۡنَآ إِنَّهَا لَمِنَ ٱلۡغَٰبِرِينَ

Ama yule mke wake aliye kafiri, tumepitisha kwa amri ya Mwenyezi Mungu kumwangamiza pamoja na watakaosalia kwenye adhabu.»

Ayah 60

فَلَمَّا جَآءَ ءَالَ لُوطٍ ٱلۡمُرۡسَلُونَ

Basi walipofika kwa Lūṭ Malaika waliotumwa

Ayah 61

قَالَ إِنَّكُمۡ قَوۡمࣱ مُّنكَرُونَ

Aliwaambia, «Kwa kweli, nyinyi ni watu msiojulikana na mimi.»

Ayah 62

قَالُواْ بَلۡ جِئۡنَٰكَ بِمَا كَانُواْ فِيهِ يَمۡتَرُونَ

Wakasema, «Usiogope. Kwani hakika yetu sisi tumekujilia na adhabu ambayo jamaa zako walikuwa na shaka nayo na hawakuwa wakiikubali kuwa ni kweli

Ayah 63

وَأَتَيۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ وَإِنَّا لَصَٰدِقُونَ

Na tumekujia na haki kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kwa hakika sisi ni wasema kweli

Ayah 64

فَأَسۡرِ بِأَهۡلِكَ بِقِطۡعࣲ مِّنَ ٱلَّيۡلِ وَٱتَّبِعۡ أَدۡبَٰرَهُمۡ وَلَا يَلۡتَفِتۡ مِنكُمۡ أَحَدࣱ وَٱمۡضُواْ حَيۡثُ تُؤۡمَرُونَ

Kwa hivyo, toka miongoni mwao , wakiwa pamoja na wewe watu wako waumini, baada ya kupita sehemu ya usiku. Na wewe nenda nyuma yao isije mmoja wao akasalia nyuma ikampata adhabu. Na jichungeni asije mmoja wenu akageuka na akatazama nyuma yake asije akaona adhabu na pia naye ikampata. Na kimbilieni kule ambako Amewaamrisha Mwenyezi Mungu, ili mpate kuwa mahali salama penye amani

Ayah 65

وَقَضَيۡنَآ إِلَيۡهِ ذَٰلِكَ ٱلۡأَمۡرَ أَنَّ دَابِرَ هَٰٓؤُلَآءِ مَقۡطُوعࣱ مُّصۡبِحِينَ

Na tukampelekea wahyi Lūṭ kwamba watu wako(waliokukanusha) wataangamizwa wote, hakuna atakayesalia, pindi kutakapoanza kupambazuka

Ayah 66

وَجَآءَ أَهۡلُ ٱلۡمَدِينَةِ يَسۡتَبۡشِرُونَ

Na wakaja wakazi wa mji wa Lūṭ mpaka kwa Lūṭ pindi walipojua kwamba kwake kuna wageni, huku wana furaha na nderemo kwa wageni wake, ili wawachukue wafanye nao machafu

Ayah 67

قَالَ إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ ضَيۡفِي فَلَا تَفۡضَحُونِ

Lūṭ akawaambia, «Hawa ni wageni wangu, na wako kwenye himaya yangu, basi msiniaziri

Ayah 68

وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلَا تُخۡزُونِ

na yaogopeni mateso ya Mwenyezi Mungu, wala msiwasumbue mkaniingiza kwenye unyonge na madharau kwa kuwaudhi wageni wangu.»

Ayah 69

قَالُوٓاْ أَوَلَمۡ نَنۡهَكَ عَنِ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Watu wake wakasema, «Kwani sisi si tulikukataza kumkaribisha mgeni yoyote miongoni mwa walimwengu - na walikuwa wakiwakatia njia wasafiri - kwa kuwa sisi tunataka kufanya machafu na wao?»

Ayah 70

قَالَ هَٰٓؤُلَآءِ بَنَاتِيٓ إِن كُنتُمۡ فَٰعِلِينَ

Lūṭ akasema kuwaambia, «Hawa wanawake wenu ni mabinti zangu, waoeni iwapo mnataka kumaliza hamu zenu, wala msiyafanye mliyokatazwa na Mwenyezi Mungu ya kuwajia wanaume.» Amewaita hao wanawake kuwa ni mabinti zake, kwa kuwa Nabii wa ummah ana cheo cha baba kwao

Ayah 71

لَعَمۡرُكَ إِنَّهُمۡ لَفِي سَكۡرَتِهِمۡ يَعۡمَهُونَ

Muumba Anaapa kwa Anayemtaka na kwa Anachokitaka. Ama muumbwa haifai kwake kuapa isipokuwa kwa jina la Mwenyezi mungu. Na Ameapa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kwa uhai wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, kwa kumtukuza kwa watu, kwamba watu wa Lūṭ wako kwenye sahau kali, wana shaka na wako kwenye ushindani

Ayah 72

فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّيۡحَةُ مُشۡرِقِينَ

Walikuwa hivyo mpaka kilipowashukia kimondo cha adhabu katika kipindi cha kutoka jua

Ayah 73

فَجَعَلۡنَا عَٰلِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمۡطَرۡنَا عَلَيۡهِمۡ حِجَارَةࣰ مِّن سِجِّيلٍ

Hapo tulivipindua vijiji vyao tukavifanya juu yake kuwa chini yake, na tukawanyeshea mawe ya udongo uliokauka ulio mgumu

Ayah 74

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتࣲ لِّلۡمُتَوَسِّمِينَ

Kwa hakika, katika yale yaliyopwapata pana mawaidha kwa wenye kuangalia na kuzingatia

Ayah 75

وَإِنَّهَا لَبِسَبِيلࣲ مُّقِيمٍ

Na kwa hakika, vijiji vyao viko kwenye njia ya kudumu ambayo wasafiri wanaopitia huko wanaviona

Ayah 76

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةࣰ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ

Kwa hakika, katika kule kuwaangamiza kwetu pana ushahidi waziwazi kwa wenye kuamini na wenye kutenda matendo yanayoambatana na sheria za Mwenyezi Mungu

Ayah 77

وَإِن كَانَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأَيۡكَةِ لَظَٰلِمِينَ

Na kwa hakika, wakazi wa mji uliozingirwa na miti, nao ni watu wa Shu'ayb, walikuwa ni wenye kuzidhulumu nafsi zao kwa kumkanusha Mwenyezi Mungu na Mtume wao mtukufu

Ayah 78

فَٱنتَقَمۡنَا مِنۡهُمۡ وَإِنَّهُمَا لَبِإِمَامࣲ مُّبِينࣲ‏

Hivyo basi tuliwaadhibu kwa mtetemeko na adhabu ya siku ya uvuli. Na kwa hakika, makazi ya watu wa Lūṭ na watu wa Shu'ayb yako katika njia iliyo wazi, watu wanayapitia katika safari zao na wanapata mazingatio

Ayah 79

وَلَقَدۡ كَذَّبَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡحِجۡرِ ٱلۡمُرۡسَلِينَ

Na kwa hakika, walimkanusha Mtume Ṣāliḥ, amani imshukiye, watu wa bonde la Hijr, nao ni kina Thamūd, wakawa kwahilo ni wenye kuwakanusha Mitume wote. Kwani mwenye kumkanusha Mtume mmoja huwa amewakanusha Mitume wote, kwani wao wako kwenye Dini moja

Ayah 80

وَءَاتَيۡنَٰهُمۡ ءَايَٰتِنَا فَكَانُواْ عَنۡهَا مُعۡرِضِينَ

Na tuliwapa watu wa Ṣāliḥ aya zetu zinazojulisha usahihi wa mambo ya haki ambayo amekuja nayo kwao Mtume Ṣāliḥ, na miongoni mwayo ni ngamia, waszingatie kwa aya hizo na wakawa ni wenye kujiweka mbali nazo na kuzipa mgongo

Ayah 81

وَكَانُواْ يَنۡحِتُونَ مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتًا ءَامِنِينَ

Na walikuwa wakiyachonga majabali na wakifanya humo majumba, na huku wao wanajiaminisha kwamba hayatawaangukia na hayataharibika

Ayah 82

فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّيۡحَةُ مُصۡبِحِينَ

Kikawachukua wao kimondo cha adhabu kipindi cha kucha mapema

Ayah 83

فَمَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ

Na hazikuwatetea wao mali zao wala zile ngome kwenye mlilima ya mawe wala zile nguvu na heshima walizopewa

Ayah 84

وَمَا خَلَقۡنَا ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَآ إِلَّا بِٱلۡحَقِّۗ وَإِنَّ ٱلسَّاعَةَ لَأٓتِيَةࣱۖ فَٱصۡفَحِ ٱلصَّفۡحَ ٱلۡجَمِيلَ

Na hatukuumba mbingu na ardhi na vilivyoko baina yake isipokuwa kwa haki, zikiwa ni zenye kujulisha ukamilifu wa muumba wake na uweza Wake, na kwamba Yeye Ndiye Ambaye ibada yoyote haifai kufanyiwa isipokuwa Yeye, Peke Yake, Asiyekuwa na mshirika. Na ule wakati ambao Kiyama kitasimama hauna budi ni wenye kuja, ili kila mtu apate kulipwa kwa yale aliyoyatenda. Basi wasamehe, ewe Mtume, hao washirikina, usiwachukulie na uyaachilie mbali wanayoyatenda

Ayah 85

إِنَّ رَبَّكَ هُوَ ٱلۡخَلَّٰقُ ٱلۡعَلِيمُ

Hakika Mola wako Ndiye Muumba wa kila kitu, Ndiye Anayekijua, kwa hivyo hakuna kitu chochote kinachomshinda wala kufichika Kwake katika ardhi wala mbinguni

Ayah 86

وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَٰكَ سَبۡعࣰ ا مِّنَ ٱلۡمَثَانِي وَٱلۡقُرۡءَانَ ٱلۡعَظِيمَ

Na kwa kweli tumekupa, ewe Mtume, ufunguo wa Qur,ani, nao ni hizo aya saba (za sura ya Fatiha) zinazokaririwa katika kila Swala, na tumekupa Qur,ani tukufu

Ayah 87

لَا تَمُدَّنَّ عَيۡنَيۡكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعۡنَا بِهِۦٓ أَزۡوَٰجࣰ ا مِّنۡهُمۡ وَلَا تَحۡزَنۡ عَلَيۡهِمۡ وَٱخۡفِضۡ جَنَاحَكَ لِلۡمُؤۡمِنِينَ

Usiziangalie kwa macho yako mawili zile starehe za duniani ambazo tuliwastarehesha nazo makafiri aina mbalimbali, na usisikitike juu ya ukafiri wao, na uwanyenyekee wenye kumuamini MwenyeziMungu na Mtume wake

Ayah 88

وَقُلۡ إِنِّيٓ أَنَا ٱلنَّذِيرُ ٱلۡمُبِينُ

Na sema, «Mimi ndiye muonyaji mwenye kuyafunua wazi yale ambayo watu wanaongokea kwayo kwenye kumuamini Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu

Ayah 89

كَمَآ أَنزَلۡنَا عَلَى ٱلۡمُقۡتَسِمِينَ

Na ni mwenye kuwaonya nyinyi isije ikawapata adhabu kama ile Aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu kwa wale walioigawanya Qur,ani, wakaiamini baadhi yake na wakaikanusha baadhi nyingine miongoni mwa Mayahudi, Wanaswara na makafiri wa Kikureshi

Ayah 90

ٱلَّذِينَ جَعَلُواْ ٱلۡقُرۡءَانَ عِضِينَ

«Na wao ni wale walioifanya Qur’ani kuwa ni vigawannyo na mafungu.» Kati yao kuna wanaosema, ‘ni uchawi’ na kati yao kuna wanaosema, ‘ni ukuhani’ na kati yao kuna wanaosema yasiyokuwa hayo ili wawazuie watu kufuata uongofu

Ayah 91

فَوَرَبِّكَ لَنَسۡـَٔلَنَّهُمۡ أَجۡمَعِينَ

Naapa kwa Mola wako, tutawahesabu tena tutawahesabu Siku ya Kiyama, na tutawalipa tena tutawalipa wote kwa kuigawanya kwao Qur’ani, kwa kuzua kwao urongo, kuibadilisha, kuipotoa na yasiyokuwa hayo

Ayah 92

عَمَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

ambayo wao walikuwa wakiyatenda ya kuabudu mizimu, maasia na madhambi. Na katika haya pana kuwatisha na kuwaonya wao wasidumu nayo haya matendo mabaya

Ayah 93

فَٱصۡدَعۡ بِمَا تُؤۡمَرُ وَأَعۡرِضۡ عَنِ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Na utangaze waziwazi ulinganizi wa haki ambao Amekuamrisha nao Mwenyezi Mungu, wala usiwajali washirikina, kwani kwa kweli Amekutakasa Mwenyezi Mungu kutokana na hayo wanayoyasema

Ayah 94

إِنَّا كَفَيۡنَٰكَ ٱلۡمُسۡتَهۡزِءِينَ

Sisi, kwa hakika, tumekutosheleza hao wacheza shere wenye kufanya dharau kati ya viongozi wa Kikureshi

Ayah 95

ٱلَّذِينَ يَجۡعَلُونَ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَۚ فَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ

ambao wameifanya mizimu na vinginevyo kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu. Basi watakuja kuujua mwisho wa vitendo vyao, hapa duniani na kesho Akhera

Ayah 96

وَلَقَدۡ نَعۡلَمُ أَنَّكَ يَضِيقُ صَدۡرُكَ بِمَا يَقُولُونَ

Na kwa kweli, tunaujua unyongekaji wa kifua chako, ewe Mtume, kwa yale wayasemayo washirikina kuhusu wewe na kuhusu ulinganizi wako

Ayah 97

فَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ وَكُن مِّنَ ٱلسَّٰجِدِينَ

Kimbilia kwa Mola wako pindi unaponyongeka moyo wako, na uitakase dhati Yake kwa kumshukuru na kumsifu. Na uwe ni miongoni mwa wenye kuswali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na wenye kumuabudu, kwani kwa kweli hilo litakutosheleza na lile lenye kukutia kero

Ayah 98

وَٱعۡبُدۡ رَبَّكَ حَتَّىٰ يَأۡتِيَكَ ٱلۡيَقِينُ

Na uendelee kumuabudu Mola wako muda wa uhai wako mpaka ikujie yakini isiyokuwa na shaka nayo ni kifu. Na Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, alitekeleza amri ya Mola Wake, kwani hakuacha kuendelea kumuabudu Mwenyezi Mungu mpaka ikamjia yakini ya kifo kutoka kwa Mola Wake

Ayah 99