Surah Al-Waaqia — The Inevitable
Surah Al-Waaqia (The Inevitable) — 56/114 · 96 aya. Soma na usikilize kwa maandishi ya Kiarabu na tafsiri ya Kiswahili.
إِذَا وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ
Kitakaposimama Kiyama
Ayah 1لَيۡسَ لِوَقۡعَتِهَا كَاذِبَةٌ
Hakutakuwa na yoyote mwenye kukanusha kusimama kwake
Ayah 2خَافِضَةࣱ رَّافِعَةٌ
Ni chenye kuwainamisha chini maadui wa Mwenyezi Mungu ndani ya Moto na ni chenye kuwainua juu Peponi wale wenye kumtegemea
Ayah 3إِذَا رُجَّتِ ٱلۡأَرۡضُ رَجࣰّ ا
Itakapotikiswa ardhi mtikiso wa nguvu
Ayah 4وَبُسَّتِ ٱلۡجِبَالُ بَسࣰّ ا
Na yakamumunyuliwa majabali mmumunyuo wa kina
Ayah 5فَكَانَتۡ هَبَآءࣰ مُّنۢبَثࣰّ ا
Yakawa vumbi lenye kuruka angani lililosukumwa na upepo
Ayah 6وَكُنتُمۡ أَزۡوَٰجࣰ ا ثَلَٰثَةࣰ
Na mkawa, enyi viumbe, makundi matatu
Ayah 7فَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ
Kundi la watu wa upande wa kulia, wenye daraja kubwa. Ni kikubwa kilioje cheo chao
Ayah 8وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ
Kuna na kundi la watu wa upande wa kushoto, wenye daraja duni. Ni mbaya iliyoje hali yao
Ayah 9وَٱلسَّٰبِقُونَ ٱلسَّٰبِقُونَ
Na wale waliotangulia mbele kwenye kheri duniani ndio wenye kutangulia mbele kwenye daraja za juu huko Akhera
Ayah 10أُوْلَٰٓئِكَ ٱلۡمُقَرَّبُونَ
Wao ndio walioletwa karibu kwa Mwenyezi Mungu
Ayah 11فِي جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ
Mola wao Atawatia kwenye mabustani ya Pepo ya starehe
Ayah 12ثُلَّةࣱ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ
Watayaingia watu wengi watu wa mwanzo wa ummah huu, na ummah wengineo wasiokuwa wao
Ayah 13وَقَلِيلࣱ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ
na wachache miongoni mwa watu mwisho wa ummah huu
Ayah 14عَلَىٰ سُرُرࣲ مَّوۡضُونَةࣲ
wakiwa juu ya vitanda vilivyofumwa kwa dhahabu
Ayah 15مُّتَّكِـِٔينَ عَلَيۡهَا مُتَقَٰبِلِينَ
na wakiwa katika hali ya kuvitegemea na huku wanaelekeana na kukutana
Ayah 16يَطُوفُ عَلَيۡهِمۡ وِلۡدَٰنࣱ مُّخَلَّدُونَ
Wanawazunguka wao kuwatumikia watumishi vijana wasiozeeka wala kufa
Ayah 17بِأَكۡوَابࣲ وَأَبَارِيقَ وَكَأۡسࣲ مِّن مَّعِينࣲ
wakiwa na vikombe, mabirika na gilasi kutoka kwenye chemchemi ya pombe yenye kupita ndani ya Pepo
Ayah 18لَّا يُصَدَّعُونَ عَنۡهَا وَلَا يُنزِفُونَ
na hawaumwi na vichwa kutokana nayo wala hawarukwi na akili
Ayah 19وَفَٰكِهَةࣲ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ
Na watawazunguka wao watumishi vijana na kila kitu wanachokichagua miongoni mwa matunda
Ayah 20وَلَحۡمِ طَيۡرࣲ مِّمَّا يَشۡتَهُونَ
nyama ya ndege ambayo nafsi zao inavutika nayo
Ayah 21وَحُورٌ عِينࣱ
Na watakuwa na wanawake wenye macho makubwa kama kwamba wao
Ayah 22كَأَمۡثَٰلِ ٱللُّؤۡلُوِٕ ٱلۡمَكۡنُونِ
kwa usafi wao na uzuri wao, ni lulu iliyohifadhiwa ndani ya mashaza yake
Ayah 23جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
hali hayo yakiwa ni malipo yao kwa yale waliokuwa wakiyafanya duniani
Ayah 24لَا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوࣰ ا وَلَا تَأۡثِيمًا
Hawatasikia humo Peponi ubatilifu wala yale ya kuwatia madhambini kuyasikia
Ayah 25إِلَّا قِيلࣰ ا سَلَٰمࣰ ا سَلَٰمࣰ ا
isipokuwa maneno yasiyokuwa na kasoro hizi na kusalimiana wao kwa wao
Ayah 26وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ
Na watu wa upande wa kulia
Ayah 27فِي سِدۡرࣲ مَّخۡضُودࣲ
ni kikubwa kilioje cheo chao na malipo yao
Ayah 28وَطَلۡحࣲ مَّنضُودࣲ
Watakuwa kwenye mikunazi isiyo na miba, na ndizi zilizopandana na kupangika
Ayah 29وَظِلࣲّ مَّمۡدُودࣲ
kila ndizi juu ya nyingine, na vivuli vya daima visivyoondoka
Ayah 30وَمَآءࣲ مَّسۡكُوبࣲ
na maji yanayotembea yasiyokatika
Ayah 31وَفَٰكِهَةࣲ كَثِيرَةࣲ
na matunda mengi
Ayah 32لَّا مَقۡطُوعَةࣲ وَلَا مَمۡنُوعَةࣲ
yasiyomalizika wala kuwaishia wala hakuna kizuizi chochote kinachowazuia wao kuyafikia
Ayah 33وَفُرُشࣲ مَّرۡفُوعَةٍ
na matandiko yaliyoinuliwa juu ya vitanda
Ayah 34إِنَّآ أَنشَأۡنَٰهُنَّ إِنشَآءࣰ
Sisi tumewaumba wanawake wa watu wa Peponi umbile ambalo silo lile umbile lililokuwa duniani, umbile lililokamilika lisilokubali kutoweka
Ayah 35فَجَعَلۡنَٰهُنَّ أَبۡكَارًا
na tumewafanya ni wanawali wenye kujipendekeza kwa waume zao
Ayah 36عُرُبًا أَتۡرَابࣰ ا
hali ya kuwa ni marika na wao kimiaka
Ayah 37لِّأَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ
Tumewaumbia wanawake hao watu wa upande wa kulia
Ayah 38ثُلَّةࣱ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ
Nao ni kundi la watu wengi wa mwanzo
Ayah 39وَثُلَّةࣱ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ
na kundi la watu wengi wa mwisho
Ayah 40وَأَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ
Na watu wa upande wa kushoto, ni mbaya iliyoje hali yao na malipo yao
Ayah 41فِي سَمُومࣲ وَحَمِيمࣲ
Watakuwa kwenye upepo ulio moto utokanao na joto la Moto wa Jahanamu utakaozuia pumzi zao, na maji moto yanayochemka
Ayah 42وَظِلࣲّ مِّن يَحۡمُومࣲ
na kivuli cha moshi mweusi sana
Ayah 43لَّا بَارِدࣲ وَلَا كَرِيمٍ
usio na mashukio baridi wala mandhari mazuri
Ayah 44إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَبۡلَ ذَٰلِكَ مُتۡرَفِينَ
Kwani wao walikuwa duniani wakijistarehesha kwa vitu vya haramu wakijiepusha na yale ambayo Mitume walikuja nayo
Ayah 45وَكَانُواْ يُصِرُّونَ عَلَى ٱلۡحِنثِ ٱلۡعَظِيمِ
Na walikuwa wamesimama wima katika kumkanusha Mwenyezi Mungu na kumshirikisha na kumuasi, na hawakuwa na nia ya kutubia kwa hayo
Ayah 46وَكَانُواْ يَقُولُونَ أَئِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابࣰ ا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ
Na walikuwa wakisema hali ya kukanusha Ufufuzi, «Je hivi sisi tutafufuliwa tutakapokufa na tukawa mchanga na mifupa iliyochakaa?» Maneno yao hayo yanaonesha kuwa wao walikuwa wakiliona jambo hili la kufufuliwa kuwa liko mbali na ukweli na wakilikanusha
Ayah 47أَوَءَابَآؤُنَا ٱلۡأَوَّلُونَ
«Je tutafufuliwa sisi na hali baba zetu waliotangulia wamekuwa mchanga uliotapakaa kwenye ardhi?»
Ayah 48قُلۡ إِنَّ ٱلۡأَوَّلِينَ وَٱلۡأٓخِرِينَ
Sema uwaambie, «Hakika wa mwanzo na wa mwisho miongoni mwa binadamu
Ayah 49لَمَجۡمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَٰتِ يَوۡمࣲ مَّعۡلُومࣲ
watakusanywa katika Siku iliyowekewa wakati maalumu, nayo ni Siku ya Kiyama
Ayah 50ثُمَّ إِنَّكُمۡ أَيُّهَا ٱلضَّآلُّونَ ٱلۡمُكَذِّبُونَ
«Kisha nyinyi, enyi mliopotea njia ya uongofu mnaokanusha onyo la Mwenyezi Mungu na agizo Lake
Ayah 51لَأٓكِلُونَ مِن شَجَرࣲ مِّن زَقُّومࣲ
ni wenye kula kutokana na mti wa zaqqūm
Ayah 52فَمَالِـُٔونَ مِنۡهَا ٱلۡبُطُونَ
nao ni katika miti mibaya zaidi, na ni wenye kujaza matumbo yenu kutokana nao kwa sababu ya ukali wa njaa
Ayah 53فَشَٰرِبُونَ عَلَيۡهِ مِنَ ٱلۡحَمِيمِ
na ni wenye kunywa juu yake maji yaliyo moto hadi ya mwisho, yasiyomaliza kiu
Ayah 54فَشَٰرِبُونَ شُرۡبَ ٱلۡهِيمِ
Mtayanywa maji hayo kwa wingi kama vile ngamia wenye kiu wasioshiba maji kwa ugonjwa uliowapata.»
Ayah 55هَٰذَا نُزُلُهُمۡ يَوۡمَ ٱلدِّينِ
Adhabu hii watakayoipata ndiyo zawadi Aliyowaandalia Siku ya Kiyama. Katika haya kuna kuwalaumu na kuwacheza shere
Ayah 56نَحۡنُ خَلَقۡنَٰكُمۡ فَلَوۡلَا تُصَدِّقُونَ
Sisi tumewaumba, enyi watu, na hamkuwa kitu chochote. Basi si msadiki kuwa kuna kufufuliwa
Ayah 57أَفَرَءَيۡتُم مَّا تُمۡنُونَ
Mnayaonaje maji ya manii mnayoyatupa ndani ya vizazi vya wake zenu
Ayah 58ءَأَنتُمۡ تَخۡلُقُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡخَٰلِقُونَ
je nyinyi ndio mnaomuumba mwanadamu kutokana na hayo au ni sisi ndio wenye kuumba
Ayah 59نَحۡنُ قَدَّرۡنَا بَيۡنَكُمُ ٱلۡمَوۡتَ وَمَا نَحۡنُ بِمَسۡبُوقِينَ
Sisi tumekadiria kifo kwenu
Ayah 60عَلَىٰٓ أَن نُّبَدِّلَ أَمۡثَٰلَكُمۡ وَنُنشِئَكُمۡ فِي مَا لَا تَعۡلَمُونَ
na sisi si wenye kushindwa kubadilisha umbo lenu Siku ya Kiyama na kuwaumba kwa sifa na namna msizozijua
Ayah 61وَلَقَدۡ عَلِمۡتُمُ ٱلنَّشۡأَةَ ٱلۡأُولَىٰ فَلَوۡلَا تَذَكَّرُونَ
Na hakika mlijua kuwa Mwenyezi Mungu Aliwaumba uumbaji wa kwanza na hamkuwa kitu chochote. Basi si mkumbuke uweza wa Mwenyezi Mungu wa kuwaumba mara nyingine
Ayah 62أَفَرَءَيۡتُم مَّا تَحۡرُثُونَ
Mnazionaje mbegu mnazozipanda
Ayah 63ءَأَنتُمۡ تَزۡرَعُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلزَّٰرِعُونَ
Je ni nyinyi mnaoziotesha kutoka ardhini? Sisi ndio tuaozituliza na kuziotesha ardhini
Ayah 64لَوۡ نَشَآءُ لَجَعَلۡنَٰهُ حُطَٰمࣰ ا فَظَلۡتُمۡ تَفَكَّهُونَ
Lau tungalitaka tungaliifanya mimea inayotokana na mbegu hizo kuwa mapepe, haimkiniki kunufaika nayo kwa kula
Ayah 65إِنَّا لَمُغۡرَمُونَ
mkawa mnaona ajabu kwa kilichoshukia mimea yenu na mnasema, «Sisi tumepata hasara na ni wenye kuungulika
Ayah 66بَلۡ نَحۡنُ مَحۡرُومُونَ
Bali sisi tumekoseshwa riziki.»
Ayah 67أَفَرَءَيۡتُمُ ٱلۡمَآءَ ٱلَّذِي تَشۡرَبُونَ
Mnayaonaje maji mnayokunywa ili mhuike kwayo
Ayah 68ءَأَنتُمۡ أَنزَلۡتُمُوهُ مِنَ ٱلۡمُزۡنِ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡمُنزِلُونَ
Je ni nyinyi mliyoyateremsha kutoka kwenye mawingu hadi kwenye kituo cha ardhi au ni sisi tuliyoyateremsha ili kuwarehemu nyinyi
Ayah 69لَوۡ نَشَآءُ جَعَلۡنَٰهُ أُجَاجࣰ ا فَلَوۡلَا تَشۡكُرُونَ
Lau tungalitaka tungaliyafanya maji haya yawe na chumvi sana, ikiwa haiwezekani kunufaika nayo kwa kunywa wala kwa mimea. Basi si mumshukuru Mola wenu kwa kuteremsha maji tamu kwa kuwanufaisha nyinyi
Ayah 70أَفَرَءَيۡتُمُ ٱلنَّارَ ٱلَّتِي تُورُونَ
Mnaouonaje moto mnaouwasha
Ayah 71ءَأَنتُمۡ أَنشَأۡتُمۡ شَجَرَتَهَآ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡمُنشِـُٔونَ
Je ni nyinyi mlioufanya mti wake, unaozalisha moto kwa kukwaruzwa, upatikane au ni sisi tulioufanya upatikane
Ayah 72نَحۡنُ جَعَلۡنَٰهَا تَذۡكِرَةࣰ وَمَتَٰعࣰ ا لِّلۡمُقۡوِينَ
Sisi tumeufanya moto wenu mnaouwasha ni ukumbusho kwenu wa Moto wa Jahanamu na pia ni manufaa kwa wasafiri
Ayah 73فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ
Basi mtakase Mola wako, ewe Nabii, Aliye mtukufu Mwenye ukamilifu wa majina na sifa, Mwingi wa wema na kheri
Ayah 74۞فَلَآ أُقۡسِمُ بِمَوَٰقِعِ ٱلنُّجُومِ
Mwenyezi Mungu Anaapa kwa mapomoko ya nyota nyakati za kuzama kwake mbinguni
Ayah 75وَإِنَّهُۥ لَقَسَمࣱ لَّوۡ تَعۡلَمُونَ عَظِيمٌ
Nacho ni kiapo kikubwa lau mnajua kadiri yake
Ayah 76إِنَّهُۥ لَقُرۡءَانࣱ كَرِيمࣱ
Hakika hii Qur’ani iliyoteremshiwa Muhammad ni Qur’ani yenye manufaa makubwa, yenye kheri nyingi na yenye elimu tele
Ayah 77فِي كِتَٰبࣲ مَّكۡنُونࣲ
iliyo ndani ya Kitabu kilichohifadhiwa, kilichofichwa na macho ya viumbe, nacho ni Kitabu ambacho kiko mikononi mwa Malaika
Ayah 78لَّا يَمَسُّهُۥٓ إِلَّا ٱلۡمُطَهَّرُونَ
Hawaigusi Qur’ani isipokuwa malaika watukufu ambao Mwenyezi Mungu Amewasafisha na aibu na madhambi. Na pia hawaigusi isipokuwa watu waliojitohirisha na ushirikina na janaba na ukosefu wa udhu
Ayah 79تَنزِيلࣱ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Na hii Qur’ani tukufu imeteremshwa kutoka kwa Mola wa viumbe vyote, kwani hiyo ndiyo haki isiyo na shaka ndani yake
Ayah 80أَفَبِهَٰذَا ٱلۡحَدِيثِ أَنتُم مُّدۡهِنُونَ
je hii Qur’ani, enyi washirikina, mnaikanusha
Ayah 81وَتَجۡعَلُونَ رِزۡقَكُمۡ أَنَّكُمۡ تُكَذِّبُونَ
Na je mnaifanya shukrani yenu kwa neema za Mola wenu ni kuwa nyinyi mnazikanusha na kukufuru? Hapa pana makaripio kwa anayedharau amri za Qur’ani na kutojali mwito wake
Ayah 82فَلَوۡلَآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلۡحُلۡقُومَ
Basi je mnaweza pindi roho ya mmoja wenu inapofika kwenye koo katika uchungu wa kifo
Ayah 83وَأَنتُمۡ حِينَئِذࣲ تَنظُرُونَ
na hali nyinyi mmehudhuria mnamtazama, kuizuia roho yake ndani ya mwili wake? Hamtaweza hilo
Ayah 84وَنَحۡنُ أَقۡرَبُ إِلَيۡهِ مِنكُمۡ وَلَٰكِن لَّا تُبۡصِرُونَ
Na sisi tuko karibu na yeye zaidi, kupitia Malaika wetu, kuliko nyinyi, lakini nyinyi hamuwaoni
Ayah 85فَلَوۡلَآ إِن كُنتُمۡ غَيۡرَ مَدِينِينَ
Na je mnaweza, iwapo nyinyi si wenye kuhesabiwa wala kulipwa kwa matendo yenu
Ayah 86تَرۡجِعُونَهَآ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
kuirudisha roho kwenye mwili, iwapo nyinyi ni wakweli? Hamtaweza kuirudisha
Ayah 87فَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ
Basi iwapo yule anayekufa ni kati ya watu wa upande wa kulia, atapata rehema kunjufu na furaha
Ayah 88فَرَوۡحࣱ وَرَيۡحَانࣱ وَجَنَّتُ نَعِيمࣲ
wakati wa kufa kwake, na kila kinachoifurahisha nafsi yake, Na atapata Pepo ya starehe huko Akhera
Ayah 89وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ
Na iwapo yule anayekufa ni kati ya watu wa upande wa kulia
Ayah 90فَسَلَٰمࣱ لَّكَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ
ataambiwa, «Umesalimika na kuwa kwenye amani, kwa kuwa wewe ni miongoni mwa watu wa upande wa kulia.»
Ayah 91وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُكَذِّبِينَ ٱلضَّآلِّينَ
Na iwapo yule anayekufa ni miongoni mwa wenye kukanusha kufufuliwa, waliopotoka na njia ya uongofu
Ayah 92فَنُزُلࣱ مِّنۡ حَمِيمࣲ
basi atapata makaribisho ya kinywaji cha moto wa Jahanamu kilichochemshwa, kilicho na joto hadi ya mwisho
Ayah 93وَتَصۡلِيَةُ جَحِيمٍ
na atachomwa na Moto na aungulike na adhabu yake kali
Ayah 94إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ حَقُّ ٱلۡيَقِينِ
Hakika habari hii tumezokuelezea, ewe Mtume, ni ukweli wa yakini usio na shaka
Ayah 95فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ
Basi litakase jina la Mola wako Aliyetukuka na umtakase na yale ambayo madhalimu na wenye kukanusha wanayasema. Mwenyezi Mungu Yuko juu ya yale wanayoyasema ujuu mkubwa sana
Ayah 96