Surah Al-Qaari'a — The Calamity

Surah Al-Qaari'a (The Calamity) — 101/114 · 11 aya. Soma na usikilize kwa maandishi ya Kiarabu na tafsiri ya Kiswahili.

ٱلۡقَارِعَةُ

Kiyama chenye kugonga nyoyo za watu kwa vituko vyake

Ayah 1

مَا ٱلۡقَارِعَةُ

Ni kitu gani hiko chenye kugonga

Ayah 2

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡقَارِعَةُ

Na ni lipi lililokujulisha ni kipi hiko chenye kugonga

Ayah 3

يَوۡمَ يَكُونُ ٱلنَّاسُ كَٱلۡفَرَاشِ ٱلۡمَبۡثُوثِ

Siku hiyo watu watakuwa , kwa wingi wao, kugawanyika kwao na kuzunguka kwao, ni kama pandzi walioenea. Nao ni wale wanaojitupa motoni

Ayah 4

وَتَكُونُ ٱلۡجِبَالُ كَٱلۡعِهۡنِ ٱلۡمَنفُوشِ

Na majabali yatakuwa ni kama pamba yenye rangi tofauti inayochambuliwa kwa mkono ikawa ni mapepe na ikamalizika

Ayah 5

فَأَمَّا مَن ثَقُلَتۡ مَوَٰزِينُهُۥ

Basi mwenye kuwa mizani za mema yake ni nzito

Ayah 6

فَهُوَ فِي عِيشَةࣲ رَّاضِيَةࣲ‏

atakuwa kwenye maisha ya kuridhika Peponi

Ayah 7

وَأَمَّا مَنۡ خَفَّتۡ مَوَٰزِينُهُۥ

Ama mwenye kuwa mizani za mema yake ni nyepesi na mizani za maovu yake ni nzito

Ayah 8

فَأُمُّهُۥ هَاوِيَةࣱ‏

makazi yake yatakuwa ni Moto wa Jahanamu

Ayah 9

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا هِيَهۡ

Ni lipi lililokujulisha, ewe Mtume, ni ipi hii Jahanamu inayoitwa «Hāwiyah»

Ayah 10

نَارٌ حَامِيَةُۢ

Ni Moto unaowaka sana kwa kuni ziliomo ndani yake

Ayah 11