Surah As-Saaffaat — Those drawn up in Ranks
Surah As-Saaffaat (Those drawn up in Ranks) — 37/114 · 182 aya. Soma na usikilize kwa maandishi ya Kiarabu na tafsiri ya Kiswahili.
وَٱلصَّٰٓفَّٰتِ صَفࣰّ ا
Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Anaapa kwa Malaika wanaojipanga, katika kuabudu kwao, mistari iliyofuatana na kushikana
Ayah 1فَٱلزَّٰجِرَٰتِ زَجۡرࣰ ا
na kwa Malaika wanaofukuza mawingu na kuyaongoza kwa amri ya MwenyeziMungu
Ayah 2فَٱلتَّٰلِيَٰتِ ذِكۡرًا
na kwa Malaika wanaosoma utajo wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na maneno Yake
Ayah 3إِنَّ إِلَٰهَكُمۡ لَوَٰحِدࣱ
kwamba muabudiwa wenu, enyi watu, ni Mmoja, Asiye na mshirika. Hivyo basi mtakasieni ibada na utiifu. Na Anaapa Mwenyezi Mungu kwa Anachotaka miongoni mwa viumbe Vyake. Ama kiumbe, hafai kuapa isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, kwani kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni ushirikina
Ayah 4رَّبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا وَرَبُّ ٱلۡمَشَٰرِقِ
Yeye Ndiye Muumba mbingu na ardhi na vilivyoko baina ya hivyo viwili, na Ndiye Mpelekeshaji jua katika sehemu zake za kuchomozea na zile za kuchwea
Ayah 5إِنَّا زَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنۡيَا بِزِينَةٍ ٱلۡكَوَاكِبِ
Sisi tumeupamba uwingu wa karibu kwa pambo la nyota
Ayah 6وَحِفۡظࣰ ا مِّن كُلِّ شَيۡطَٰنࣲ مَّارِدࣲ
Na tumeuhifadhi huo uwingu, kwa nyota, na kila shetani mwenye kuasi, mjeuri, aliyefukuzwa (kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu)
Ayah 7لَّا يَسَّمَّعُونَ إِلَى ٱلۡمَلَإِ ٱلۡأَعۡلَىٰ وَيُقۡذَفُونَ مِن كُلِّ جَانِبࣲ
Hawawezi hao Mashetani kufika kwenye viumbe vya juu, navyo ni mbingu na Malaika waliyomo ndani yake, wakapata kuwasikiliza wanapoutamka wahyi ambao Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Anauleta, unaokusanya sheria Yake na makadirio Yake, na wanavurumizwa vimondo katika kila upande
Ayah 8دُحُورࣰ اۖ وَلَهُمۡ عَذَابࣱ وَاصِبٌ
kwa kuwafukuza ili wasipate kusikiliza. Na huko kwenye Nyumba ya Akhera watakuwa na adhabu ya daima yenye kuumiza
Ayah 9إِلَّا مَنۡ خَطِفَ ٱلۡخَطۡفَةَ فَأَتۡبَعَهُۥ شِهَابࣱ ثَاقِبࣱ
Isipokuwa yule aliyenyakuwa, miongoni mwa Mashetani, mnyakuo wa haraka, nao ni lile neno analolisikia mbinguni kwa haraka, akamtupia aliyekuwa chini yake, na yule mwingine akamtupia aliyekuwa chini yake. Basi pengine huenda akafikiwa na kimondo chenye kutoa mwangaza kabla hajalitupa, na pengine huwa amelitupa kwa makadirio ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kabla ya kujiwa na kimondo kikamchoma, na yule mwingine akaenda nalo hadi kwa makuhani wakaongeza juu ya neno hilo maneno mia moja ya urongo
Ayah 10فَٱسۡتَفۡتِهِمۡ أَهُمۡ أَشَدُّ خَلۡقًا أَم مَّنۡ خَلَقۡنَآۚ إِنَّا خَلَقۡنَٰهُم مِّن طِينࣲ لَّازِبِۭ
Basi waulize, ewe Mtume, wenye kukanusha Kufufuliwa: Je kuumbwa kwao ni kugumu zaidi au ni hivyi viumbe tulivyoviumba? Kwa hakika, tulimuumba baba yao Ādam kwa udongo ulioshikana na kuambatana
Ayah 11بَلۡ عَجِبۡتَ وَيَسۡخَرُونَ
Bali ulistaajabu, ewe Mtume, kwa ukanushaji wao na kukataa kwao Kufufuliwa. Na la kustaajabiwa zaidi na lililo kubwa zaidi kuliko lile la kukataa kwao ni kwamba wao wanakucheza shere na kulidharau neno lako
Ayah 12وَإِذَا ذُكِّرُواْ لَا يَذۡكُرُونَ
Na wanapokumbushwa walichokisahau au walichoghafilika nacho, hawanufaiki kwa huo ukumbusho wala hawazingatii
Ayah 13وَإِذَا رَأَوۡاْ ءَايَةࣰ يَسۡتَسۡخِرُونَ
Na wanapoiona miujiza yenye kutolea dalili unabii wako, wanakufanyia shere na wanastaajabu
Ayah 14وَقَالُوٓاْ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرࣱ مُّبِينٌ
Na wanasema, «Halikuwa hili ulilotuletea isipokuwa ni uchawi uliojitokeza waziwazi
Ayah 15أَءِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابࣰ ا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ
Je, tunapokufa na tukawa ni mchanga na mifupa iliyochakaa, je sisi ni wenye kufufuliwa kutoka makaburini mwetu tukiwa hai
Ayah 16أَوَءَابَآؤُنَا ٱلۡأَوَّلُونَ
au pia watafufuliwa baba zetu waliopita kabla yetu?»
Ayah 17قُلۡ نَعَمۡ وَأَنتُمۡ دَٰخِرُونَ
Waambie, ewe Mtume, «Ndio mtafufuliwa hali mkiwa wanyonge, watwevu.»
Ayah 18فَإِنَّمَا هِيَ زَجۡرَةࣱ وَٰحِدَةࣱ فَإِذَا هُمۡ يَنظُرُونَ
Hakika ni kwamba huo utakuwa ni Mvuvio mmoja, wakitahamaki wao wamesimama kutoka makaburini mwao, wanatazama vituko vya Kiyama
Ayah 19وَقَالُواْ يَٰوَيۡلَنَا هَٰذَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ
Na watasema, «Ewe maangamivu yetu! Hii ni siku ya kuhesabiwa na kulipwa!»
Ayah 20هَٰذَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِ ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ
Hapo wataambiwa, «Hii ndiyo Siku ya Uamuzi wa haki baina ya viumbe, ambayo mlikuwa mkiikanusha duniani na mkiikataa.»
Ayah 21۞ٱحۡشُرُواْ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ وَأَزۡوَٰجَهُمۡ وَمَا كَانُواْ يَعۡبُدُونَ
Na Malaika wataambiwa, «Wakusanyeni wale waliomkanusha Mwenyezi Mungu na wafananao na wao na waungu wao waliokuwa wakiwaabudu
Ayah 22مِن دُونِ ٱللَّهِ فَٱهۡدُوهُمۡ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلۡجَحِيمِ
badala ya Mwenyezi Mungu, na muwasukume kwa nguvu hadi kwenye moto wa Jahanamu
Ayah 23وَقِفُوهُمۡۖ إِنَّهُم مَّسۡـُٔولُونَ
«Na muwafunge kabla hawajafika kwenye moto wa Jahanamu, kwa kuwa wao ni wenye kuulizwa kuhusu matendo yao na maneno yao yaliyotokana na wao duniani, kwa namna ya kumshtukia kuwakaripia.»
Ayah 24مَا لَكُمۡ لَا تَنَاصَرُونَ
Na wataambiwa kwa kulaumiwa, «Kwa nini hamsaidiani nyinyi kwa nyinyi?»
Ayah 25بَلۡ هُمُ ٱلۡيَوۡمَ مُسۡتَسۡلِمُونَ
Bali wao Leo ni wenye kufuata amri ya Mwenyezi Mungu, hawataenda kinyume nayo wala hawataepukana nayo, hawajisaidii wao wenyewe
Ayah 26وَأَقۡبَلَ بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضࣲ يَتَسَآءَلُونَ
Na hapo makafiri watakabiliana wao kwa wao wakilaumiana na wakigombana
Ayah 27قَالُوٓاْ إِنَّكُمۡ كُنتُمۡ تَأۡتُونَنَا عَنِ ٱلۡيَمِينِ
Wafuasi watasema kuwaambia wafuatwa, «Nyinyi mlikuwa mkitujia kwa upande wa dini na haki, mkiifanya Sheria ni twevu kwetu, mkitutia chuki nayo na mkitupambia upotevu.»
Ayah 28قَالُواْ بَل لَّمۡ تَكُونُواْ مُؤۡمِنِينَ
Hapo watasema wafuatwa kuwaabia wafuasi, «Mambo si kama vile mnavyodai, bali ni nyoyo zenu zilikuwa zimekataa kuamini, zimeuelekea ukafiri na uasi
Ayah 29وَمَا كَانَ لَنَا عَلَيۡكُم مِّن سُلۡطَٰنِۭۖ بَلۡ كُنتُمۡ قَوۡمࣰ ا طَٰغِينَ
«Na sisi hatukuwa na hoja juu yenu wala nguvu, tukaweza kwa hizo kuwazuilia kuamini. Bali nyinyi wenyewe, enyi washirikina, mlikuwa waasi wenye kupita mipaka ya haki
Ayah 30فَحَقَّ عَلَيۡنَا قَوۡلُ رَبِّنَآۖ إِنَّا لَذَآئِقُونَ
«Hivyo basi ndio sisi sote ikalazimu tupate onyo la Mola wetu kuwa ni wenye kuonja adhabu, sisi na nyinyi, kwa yale tuliyoyatanguliza ya madhambi na maasia duniani
Ayah 31فَأَغۡوَيۡنَٰكُمۡ إِنَّا كُنَّا غَٰوِينَ
« Ndipo tukawapoteza na njia ya Mwenyezi Mungu na ya kumuamini, kwa kuwa sisi wenyewe tulikuwa ni wapotevu kabla yenu. Na kwa hivyo tukapotea kwa sababu ya ukafiri wetu na tukawaangamiza nyinyi pamoja na sisi.»
Ayah 32فَإِنَّهُمۡ يَوۡمَئِذࣲ فِي ٱلۡعَذَابِ مُشۡتَرِكُونَ
Basi wafuasi na wafuatwa watashirikiana katika adhabu Siku ya Kiyama, kama walivyoshirikiana ulimwenguni katika kumuasi Mwenyezi Mungu
Ayah 33إِنَّا كَذَٰلِكَ نَفۡعَلُ بِٱلۡمُجۡرِمِينَ
Hivi ndivyo sisi tunavyowafanyia waliochagua mambo ya kumuasi Mwenyezi Mungu ulimwenguni na wakaacha kumtii, basi tutawaonjesha adhabu kali
Ayah 34إِنَّهُمۡ كَانُوٓاْ إِذَا قِيلَ لَهُمۡ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ يَسۡتَكۡبِرُونَ
Hakika wale washirikina walikuwa duniani wakiambiwa, «Hapana mola anayepasa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu,» na wakaitwa kwenye mwito huo na wakaamrishwa kuyaacha yanayopingana nao, wanaufanyia kiburi na kumfanyia kiburi aliyekuja nao
Ayah 35وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُوٓاْ ءَالِهَتِنَا لِشَاعِرࣲ مَّجۡنُونِۭ
Na wanasema, «Je, tuache kuwaabudu waungu wetu kwa maneno ya mshairi mwenye wazimu?» wakimkusudia Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie
Ayah 36بَلۡ جَآءَ بِٱلۡحَقِّ وَصَدَّقَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Wamesema urongo! Muhammad sivyo vile walivyomueleza. Bali amekuja na Qur’ani na upwekeshaji Mwenyezi Mungu, na akathibitisha ukweli wa Mitume katika kile walichokitolea habari kuhusu sheria ya Mwenyezi Mungu na kumpwekesha Yeye
Ayah 37إِنَّكُمۡ لَذَآئِقُواْ ٱلۡعَذَابِ ٱلۡأَلِيمِ
Hakika yenu nyinyi, enyi washirikina, kwa neno lenu, ukafiri wenu na kukanusha kwenu, ni wenye kuonja adhabu iliyo kali yenye uchungu
Ayah 38وَمَا تُجۡزَوۡنَ إِلَّا مَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Na hamtalipwa huko Akhera isipokuwa kwa lile la maasia mliokuwa mkilifanya duniani
Ayah 39إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ
Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, waliomtakasia Ibada Yake, Akawatakasa na Akawahusu wao kwa rehema Yake, basi hao kwa hakika ni wenye kuokoka na adhabu yenye uchungu
Ayah 40أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ رِزۡقࣱ مَّعۡلُومࣱ
Hao waliotakaswa watapata riziki ijulikanayo isiyokatika ndani ya Pepo
Ayah 41فَوَٰكِهُ وَهُم مُّكۡرَمُونَ
Riziki hiyo ni matunda aina mbalimbali. Na wao ni wenye kukirimiwa kwa takrima ya Mwenyezi Mungu
Ayah 42فِي جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ
kuwafanyia wao ndani ya mabustani ya Pepo ya starehe ya milele
Ayah 43عَلَىٰ سُرُرࣲ مُّتَقَٰبِلِينَ
Na miongoni mwa takrima yao watakayoipata kwa Mola wao, na kukirimiana wao kwa wao, ni kuwa wao watakuwa kwenye vitanda wameelekeana
Ayah 44يُطَافُ عَلَيۡهِم بِكَأۡسࣲ مِّن مَّعِينِۭ
Zinazungushwa kwao gilasi za Pombe inayotoka kwenye mito inayotembea, hawachelei kuwa itamalizika
Ayah 45بَيۡضَآءَ لَذَّةࣲ لِّلشَّٰرِبِينَ
ni nyeupe rangi yake, ni tamu katika kuinywa
Ayah 46لَا فِيهَا غَوۡلࣱ وَلَا هُمۡ عَنۡهَا يُنزَفُونَ
haina madhara yoyote ya akili wala ya mwili
Ayah 47وَعِندَهُمۡ قَٰصِرَٰتُ ٱلطَّرۡفِ عِينࣱ
Na hapo kwao kwenye makao yao watakuwako wanawake waliojihifadhi, hawawatazami isipokuwa waume zao, wazuri wa macho
Ayah 48كَأَنَّهُنَّ بَيۡضࣱ مَّكۡنُونࣱ
kama kwamba wao ni mayai yaliyotunzwa ambayo hayajaguswa na mikono
Ayah 49فَأَقۡبَلَ بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضࣲ يَتَسَآءَلُونَ
Hapo wataelekeana wakiulizana kuhusu hali zao za duniani na mambo ya usumbufu waliokuwa wakikutana nayo huko, na yale ambayo Mwenyezi Mungu Aliwaneemesha nayo Peponi. Na huku ndiko kuliwazika kuliotimia
Ayah 50قَالَ قَآئِلࣱ مِّنۡهُمۡ إِنِّي كَانَ لِي قَرِينࣱ
Atasema msemaji miongoni mwa watu wa Peponi, «Kwa kweli, nilikuwa na rafiki duniani aliyeshikana na mimi
Ayah 51يَقُولُ أَءِنَّكَ لَمِنَ ٱلۡمُصَدِّقِينَ
«Aliyekuwa akisema, ‘Ni vipi wewe unaamini Ufufuzi ambao ni upeo wa kustaajabisha
Ayah 52أَءِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابࣰ ا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَدِينُونَ
Je, tunapokufa, tukakatika vipande- vipande na tukawa mchanga na mifupa, kwani ni wenye kufufuliwa, kuhesabiwa na kulipwa kwa matendo yetu?’»
Ayah 53قَالَ هَلۡ أَنتُم مُّطَّلِعُونَ
Atasema huyu Muumini aliyetiwa Peponi akiwaambia wenzake, «Je, nyinyi ni wenye kuchungulia mpate kuona mwisho wa yule rafiki?»
Ayah 54فَٱطَّلَعَ فَرَءَاهُ فِي سَوَآءِ ٱلۡجَحِيمِ
Hapo akachungulia na akamuona rafiki yake katikati ya Moto
Ayah 55قَالَ تَٱللَّهِ إِن كِدتَّ لَتُرۡدِينِ
Muumini atasema kumwambia rafiki yake mwenye kukanusha kufufuliwa, «Ulikaribia kuniangamiza kwa kunizuia nisiamini lau nilikutii
Ayah 56وَلَوۡلَا نِعۡمَةُ رَبِّي لَكُنتُ مِنَ ٱلۡمُحۡضَرِينَ
Na lau si wema wa Mola wangu kwa kuniongoza mimi kwenye Imani na kunithibitisha juu yake, ningalikuwa ni mwenye kuhudhurishwa kwenye adhabu pamoja na wewe
Ayah 57أَفَمَا نَحۡنُ بِمَيِّتِينَ
«Je, ni kweli sisi ni wenye kukalishwa milele na kuneemeshwa, si wenye kufa
Ayah 58إِلَّا مَوۡتَتَنَا ٱلۡأُولَىٰ وَمَا نَحۡنُ بِمُعَذَّبِينَ
isipokuwa kifo chetu cha mwanzo huko ulimwenguni, na sisi si wenye kuadhibiwa baada ya kuingia kwetu Peponi
Ayah 59إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ
Hakika starehe hii tuliyo nayo ndiyo kufaulu kukubwa
Ayah 60لِمِثۡلِ هَٰذَا فَلۡيَعۡمَلِ ٱلۡعَٰمِلُونَ
«Basi kwa kupata mfano wa starehe hizi kamilifu, makazi ya daima na kufaulu kukubwa, na watende wenye kutenda duniani ili wazifikie huko Akhera.»
Ayah 61أَذَٰلِكَ خَيۡرࣱ نُّزُلًا أَمۡ شَجَرَةُ ٱلزَّقُّومِ
Je, hayo yaliyotangulia kuelezwa ya starehe za Pepo ni makaribisho bora na vipewa vya Mwenyezi Mungu, au ni mti mbaya uliolaaniwa wa zaqqūm, ambao ni chakula cha watu wa Motoni
Ayah 62إِنَّا جَعَلۡنَٰهَا فِتۡنَةࣰ لِّلظَّٰلِمِينَ
Sisi tumeufanya ni mtihani waliotahiniwa nao madhalimu kwa ukanushaji na kufanya mambo ya uasi na wakasema kwa njia ya kiburi, «Mtu wenu anawapa habari kwamba motoni kuna mti, na moto unakula miti.»
Ayah 63إِنَّهَا شَجَرَةࣱ تَخۡرُجُ فِيٓ أَصۡلِ ٱلۡجَحِيمِ
Hakika huo ni mti ambao unaota kwenye uketo wa moto wa Jahanamu, matunda yake yana sura mbaya
Ayah 64طَلۡعُهَا كَأَنَّهُۥ رُءُوسُ ٱلشَّيَٰطِينِ
kama vichwa vya Mashetani
Ayah 65فَإِنَّهُمۡ لَأٓكِلُونَ مِنۡهَا فَمَالِـُٔونَ مِنۡهَا ٱلۡبُطُونَ
Basi yanapokuwa hivyo, usiulize baada ya haya kuhusu utamu wake. Kwani washirikina ni wenye kula kutoka mti huo na ni wenye kujaza matumbo yao kwa matunda hayo
Ayah 66ثُمَّ إِنَّ لَهُمۡ عَلَيۡهَا لَشَوۡبࣰ ا مِّنۡ حَمِيمࣲ
Kisha wao, baada ya kuyala ni wenye kunywa kinywaji mchanganyiko kilicho kibaya na kilicho moto
Ayah 67ثُمَّ إِنَّ مَرۡجِعَهُمۡ لَإِلَى ٱلۡجَحِيمِ
Kisha marejeo yao baada ya adhabu hii ni kuishia (hukohuko) kwenye adhabu ya Moto
Ayah 68إِنَّهُمۡ أَلۡفَوۡاْ ءَابَآءَهُمۡ ضَآلِّينَ
Hakika wao waliwakuta baba zao kwenye ushirikina na upotevu
Ayah 69فَهُمۡ عَلَىٰٓ ءَاثَٰرِهِمۡ يُهۡرَعُونَ
na wakakimbilia kuwafuata katika hilo
Ayah 70وَلَقَدۡ ضَلَّ قَبۡلَهُمۡ أَكۡثَرُ ٱلۡأَوَّلِينَ
na kwa hakika, kabla ya watu wako, ewe Mtume, walipotea na kuwa kando na haki ummah wengi waliotangulia
Ayah 71وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا فِيهِم مُّنذِرِينَ
Na kwa hakika, tuliwatumiliza kwa ummah hao Mitume waliowaonya adhabu, lakini wakakanusha
Ayah 72فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُنذَرِينَ
Basi fikiria: ulikuwa vipi mwisho wa ummah hao walioonywa na wakakanusha? Waliadhibiwa na wakawa ni mazingatio kwa watu
Ayah 73إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ
Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu Aliyowasafisha na Akawachagua kwa kuwapa rehema Yake kwa kule kumtakasa kwao Yeye
Ayah 74وَلَقَدۡ نَادَىٰنَا نُوحࣱ فَلَنِعۡمَ ٱلۡمُجِيبُونَ
Na kwa hakika Alituita kwa kutuomba Nabii wetu Nūḥ tumlinde na watu wake, basi bora wa wenye kumuitikia tulikuwa ni sisi
Ayah 75وَنَجَّيۡنَٰهُ وَأَهۡلَهُۥ مِنَ ٱلۡكَرۡبِ ٱلۡعَظِيمِ
Na tukamuokoa yeye na watu wa nyumbani kwake na Waumini pamoja naye kutokana na maudhi ya washirikina na kutokana na kuzamishwa kwa mafuriko makubwa
Ayah 76وَجَعَلۡنَا ذُرِّيَّتَهُۥ هُمُ ٱلۡبَاقِينَ
Na tukawafanya watoto wa Nūḥ ndio wenye kusalia baada ya kuzamishwa watu wake
Ayah 77وَتَرَكۡنَا عَلَيۡهِ فِي ٱلۡأٓخِرِينَ
Na tukamuwekea utajo mwema na sifa nzuri kwa watu waliokuja baada yake wakawa wanamtaja nazo
Ayah 78سَلَٰمٌ عَلَىٰ نُوحࣲ فِي ٱلۡعَٰلَمِينَ
Amani imfikie Nūḥ na asalimike na kutajwa kwa ubaya katika kipindi cha watu wa mwisho, bali asifiwe na watu wa vizazi vinavyokuja baada yake
Ayah 79إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Mfano wa malipo mema tuliomlipa Nūḥ, tutamlipa kila aliyefanya vizuri, miongoni mwa waja, katika kumtii Mwenyezi Mungu
Ayah 80إِنَّهُۥ مِنۡ عِبَادِنَا ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Hakika Nūḥ ni miongoni mwa waja wetu wenye kuamini, wenye kumtakasia Mwenyezi Mungu na wenye kufuata amri za Mwenyezi Mungu kivitendo
Ayah 81ثُمَّ أَغۡرَقۡنَا ٱلۡأٓخَرِينَ
Kisha tukawazamisha wengine, wenye kukanusha kati ya watu wake, kwa mafuriko, kisisalie chochote, miongoni mwao, hata jicho lenye kupepesa
Ayah 82۞وَإِنَّ مِن شِيعَتِهِۦ لَإِبۡرَٰهِيمَ
Na miongoni mwa waliokuwa katika nyendo za Nūḥ, njia yake na mila yake ni Nabii wa Mwenyezi Mungu Ibrāhīm
Ayah 83إِذۡ جَآءَ رَبَّهُۥ بِقَلۡبࣲ سَلِيمٍ
alipomjia Mola wake kwa moyo uliyojitenga na kila itikadi ya ubatilifu na tabia ya kujitukanisha
Ayah 84إِذۡ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوۡمِهِۦ مَاذَا تَعۡبُدُونَ
alipomwambia babake na watu wake kwa njia ya kuwakanya, «Ni kitu gani hiko mnachokiabudu badala ya Mwenyezi Mungu
Ayah 85أَئِفۡكًا ءَالِهَةࣰ دُونَ ٱللَّهِ تُرِيدُونَ
Je, mnataka kuabudu waungu wa kuzuliwa na mnaacha kumuabudu Mwenyezi Mungu Anayestahiki kuabudiwa Peke Yake
Ayah 86فَمَا ظَنُّكُم بِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Mnamdhani Mola wa viumbe vyote Atawafanya nini mkimshirikisha Yeye na mkamuabudu asiyekuwa Yeye
Ayah 87فَنَظَرَ نَظۡرَةࣰ فِي ٱلنُّجُومِ
Akatazama mtazamo mmoja kwenye nyota kulingana na mila ya watu wake kuhusu hilo, huku akifikiria udhuru wa kuutoa ili asipate kutoka na wao kwenda kwenye sherehe zao
Ayah 88فَقَالَ إِنِّي سَقِيمࣱ
akawaambia, «Mimi ni mgonjwa.» Hii ilikuwa ni ishara ya mbali kutoka kwake
Ayah 89فَتَوَلَّوۡاْ عَنۡهُ مُدۡبِرِينَ
Basi wakamuacha nyuma yao
Ayah 90فَرَاغَ إِلَىٰٓ ءَالِهَتِهِمۡ فَقَالَ أَلَا تَأۡكُلُونَ
Akabeta kwa haraka kuelekea kwenye masanamu wa watu wake, akasema kwa njia ya kuwakejeli, «Si mkile chakula hiki ambacho washika mlango wenu wanawapatia
Ayah 91مَا لَكُمۡ لَا تَنطِقُونَ
Muna nini nyinyi mbona hamsemi wala hamumjibu mwenye kuwaomba
Ayah 92فَرَاغَ عَلَيۡهِمۡ ضَرۡبَۢا بِٱلۡيَمِينِ
Akawaelekea waungu wao kuwapiga na kuwavunja-vunja kwa mkono wake wa kulia, ili kuwathibitishia makosa ya kuwaabudu
Ayah 93فَأَقۡبَلُوٓاْ إِلَيۡهِ يَزِفُّونَ
Wakaja kumkabili kwa haraka na mbio huku wana hasira
Ayah 94قَالَ أَتَعۡبُدُونَ مَا تَنۡحِتُونَ
Ibrāhīm akakutana na wao akiwa imara kwa kusema, «Vipi mtaabudu masanamu mnaowachonga nyinyi wenyewe na mnaowatengeneza kwa mikono yenu
Ayah 95وَٱللَّهُ خَلَقَكُمۡ وَمَا تَعۡمَلُونَ
na mnaacha kumuabudu Mola wenu Aliyewaumba nyinyi na Akayaumba matendo yenu?»
Ayah 96قَالُواْ ٱبۡنُواْ لَهُۥ بُنۡيَٰنࣰ ا فَأَلۡقُوهُ فِي ٱلۡجَحِيمِ
Hoja ilipowasimamia, waliamua kutumia nguvu na wakasema, «Jengeni jengo kwa ajili yake, mlijaze kuni kisha mumtupe ndani yake»
Ayah 97فَأَرَادُواْ بِهِۦ كَيۡدࣰ ا فَجَعَلۡنَٰهُمُ ٱلۡأَسۡفَلِينَ
Watu wa Ibrāhīm wakataka kumfanyia vitimbi ili wamuangamize, tukawafanya wao kuwa ndio wenye kutendeshwa nguvu na kushindwa. Mwenyezi Mungu Akavirudisha vitimbi vyao kwenye shingo zao na akaufanya ule moto uwe baridi na salama kwa Ibrāhīm
Ayah 98وَقَالَ إِنِّي ذَاهِبٌ إِلَىٰ رَبِّي سَيَهۡدِينِ
Akasema Ibrāhīm, «Mimi nahamia kwa Mola wangu kutoka kwenye mji wa watu wangu kuelekea pale ambapo nitamakinika kumuabudu Mola wangu, kwani Yeye Atanielekeza kwenye kheri ya Dini yangu na dunia yangu
Ayah 99رَبِّ هَبۡ لِي مِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ
Mola wangu! Nipe mtoto mwema.»
Ayah 100فَبَشَّرۡنَٰهُ بِغُلَٰمٍ حَلِيمࣲ
Tukamkubalia ombi lake na tukambashiria kuwa atapata mtoto wa kiume atakayekuwa mpole ukubwani mwake, naye ni Ismā'īl
Ayah 101فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ ٱلسَّعۡيَ قَالَ يَٰبُنَيَّ إِنِّيٓ أَرَىٰ فِي ٱلۡمَنَامِ أَنِّيٓ أَذۡبَحُكَ فَٱنظُرۡ مَاذَا تَرَىٰۚ قَالَ يَٰٓأَبَتِ ٱفۡعَلۡ مَا تُؤۡمَرُۖ سَتَجِدُنِيٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلصَّٰبِرِينَ
Alipokuwa mkubwa Ismā'īl, akawa anatembea na babake, babake alimwambia, «Mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja, je, una maoni gani?» (na ndoto za Manabii ni za kweli). Ismā'īl akasema, kwa kumridhisha Mola wake, kumtii mzazi wake na kumsaidia juu ya utiifu wa Mwenyezi Mungu, «Endelea katika jambo Alilokuamrisha Mwenyezi Mungu la kunichinja mimi. Utanikuta, Mwenyezi Mungu Akitaka, ni mvumilivu, mtiifu na ni mwenye kutarajia malipo mema (kutoka kwa Mwenyezi Mungu)»
Ayah 102فَلَمَّآ أَسۡلَمَا وَتَلَّهُۥ لِلۡجَبِينِ
Walipojisalimisha wao wawili kwa kuifuata amri ya Mwenyezi Mungu na kuiandama, na Ibrāhīm akambwaga Ismā'īl chini, kwa upande wa paji la uso, ili kumchinja
Ayah 103وَنَٰدَيۡنَٰهُ أَن يَٰٓإِبۡرَٰهِيمُ
Na tukamuita Ibrāhīm katika hali hiyo ngumu kwamba: Ewe Ibrāhīm! Umeshalifanya uliloamrishwa na, kwa hivyo
Ayah 104قَدۡ صَدَّقۡتَ ٱلرُّءۡيَآۚ إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ
umeisadikisha ndoto yako. Hakika yetu sisi kama vile tulivyokulipa mema kwa kuamini kwako , ndivyo tunavyowalipa wale waliofanya wema mfano wako, tuwaepushie shida duniani na Akhera
Ayah 105إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ ٱلۡبَلَٰٓؤُاْ ٱلۡمُبِينُ
Hakika amri ya kuwa wewe umuue mwano ndio mtihani mgumu uliodhihirisha ukweli wa Imani yako
Ayah 106وَفَدَيۡنَٰهُ بِذِبۡحٍ عَظِيمࣲ
Na tukamuokoa Ismā'īl, na tukamuekea kondoo mkubwa kuwa ni badala yake
Ayah 107وَتَرَكۡنَا عَلَيۡهِ فِي ٱلۡأٓخِرِينَ
Na tukambakishia Ibrāhīm baada yake sifa njema kwa watu
Ayah 108سَلَٰمٌ عَلَىٰٓ إِبۡرَٰهِيمَ
Maamkizi kwa Ibrāhīm kutoka kwa Mola wake na kumuombea asalimike na kila dhara
Ayah 109كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Kama tulivyomlipa malipo mema Ibrāhīm kwa utiifu wake kwetu na kufuata kwake amri yetu, ndivyo tutakavyowalipa wenye kufanya wema miongoni mwa waja wetu
Ayah 110إِنَّهُۥ مِنۡ عِبَادِنَا ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Hakika yeye ni miongoni mwa waja wetu Waumini waliyoipa hiyo sifa ya uja haki yake
Ayah 111وَبَشَّرۡنَٰهُ بِإِسۡحَٰقَ نَبِيࣰّ ا مِّنَ ٱلصَّٰلِحِينَ
Na tukampa bishara Ibrāhīm ya mtoto wake, Isḥāq, kuwa atakuwa Nabii, miongoni mwa watu wema. Hayo yakiwa ni malipo ya uvumilivu wake na kuridhika kwake na amri ya Mola wake na utiifu wake Kwake
Ayah 112وَبَٰرَكۡنَا عَلَيۡهِ وَعَلَىٰٓ إِسۡحَٰقَۚ وَمِن ذُرِّيَّتِهِمَا مُحۡسِنࣱ وَظَالِمࣱ لِّنَفۡسِهِۦ مُبِينࣱ
Na tukawateremshia baraka. Na miongoni mwa wale wanaotokana na kizazi chao kuna anayemtii Mola wake, anayeifanyia wema nafsi yake, na kuna anayeidhulumu (nafsi yake) dhulma iliyo wazi kwa ukafiri wake na utendaji wake maasia
Ayah 113وَلَقَدۡ مَنَنَّا عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَٰرُونَ
Na kwa hakika tuliwafanyia wema Mūsā na Hārūn kwa kuwapa unabii na utume
Ayah 114وَنَجَّيۡنَٰهُمَا وَقَوۡمَهُمَا مِنَ ٱلۡكَرۡبِ ٱلۡعَظِيمِ
Na tukawaokoa wao wawili na watu wao kutokana na gharika, utumwa na unyonge waliokuwa nao
Ayah 115وَنَصَرۡنَٰهُمۡ فَكَانُواْ هُمُ ٱلۡغَٰلِبِينَ
Na tukawanusuru, wakawa na enzi, usaidizi na ushindi juu ya Fir'awn na jamaa zake
Ayah 116وَءَاتَيۡنَٰهُمَا ٱلۡكِتَٰبَ ٱلۡمُسۡتَبِينَ
Na tukawapa wao wawili Taurati yenye ufafanuzi
Ayah 117وَهَدَيۡنَٰهُمَا ٱلصِّرَٰطَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ
na tukawaongoza njia iliyonyoka isiyokuwa na upotovu, nayo ni Uislamu, Dini ya Mwenyezi Mungu ambayo Amewatumiliza Manabii Wake kwayo
Ayah 118وَتَرَكۡنَا عَلَيۡهِمَا فِي ٱلۡأٓخِرِينَ
na tukazifanya sifa zao nzuri na utajo wao mwema ni vyenye kusalia baada yao
Ayah 119سَلَٰمٌ عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَٰرُونَ
Maamkizi kwa Mūsā na Hārūn kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na sifa njema na kuwaombea wao wasalimike na kila dhara
Ayah 120إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Kama tulivyowalipa wao malipo mema , ndivyo tutakavyowalipa wenye kufanya wema miongoni mwa waja wetu wenye kututakasia kwa ukweli, kuamini na kutenda
Ayah 121إِنَّهُمَا مِنۡ عِبَادِنَا ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Hakika ya wao wawili ni miongoni mwa waja wetu waliojikita katika Imani
Ayah 122وَإِنَّ إِلۡيَاسَ لَمِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Na hakika mja wetu Ilyas ni miongoni mwa wale ambao tuliwakirimu kwa unabii na utume
Ayah 123إِذۡ قَالَ لِقَوۡمِهِۦٓ أَلَا تَتَّقُونَ
Kumbuka na utaja pindi aliposema kuwaambia watu wake, kati ya Wana wa Isrāīl, «Mcheni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, na mumuogope, na msimshirikishe mwengine pamoja na Yeye
Ayah 124أَتَدۡعُونَ بَعۡلࣰ ا وَتَذَرُونَ أَحۡسَنَ ٱلۡخَٰلِقِينَ
Vipi nyinyi mtaliabudu sanamu ambalo ni kiumbe dhaifu na mtamuacha Mzuri wa kuumba, Mwenye sifa nzuri na kamilifu kabisa
Ayah 125ٱللَّهَ رَبَّكُمۡ وَرَبَّ ءَابَآئِكُمُ ٱلۡأَوَّلِينَ
mkawa hamtamuabudu Mwenyezi Mungu Ambaye ni Mola wenu Aliyewaumba nyinyi na Akawaumba baba zenu waliopita kabla yenu?»
Ayah 126فَكَذَّبُوهُ فَإِنَّهُمۡ لَمُحۡضَرُونَ
Watu wa Ilyas walimkanusha Nabii wao. Basi Mwenyezi Mungu , kwa hakika, Atawakusanya Siku ya Kiyama ili wahesabiwe na wateswe
Ayah 127إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ
Isipokuwa wale waja wa Mwenyezi Mungu waliomtakasia Mwenyezi Mungu Dini yao, basi hao ni wenye kuokoka na adhabu Yake
Ayah 128وَتَرَكۡنَا عَلَيۡهِ فِي ٱلۡأٓخِرِينَ
Tulimfanya Ilyas awe na sifa nzuri kwa ummah waliokuja baada yake
Ayah 129سَلَٰمٌ عَلَىٰٓ إِلۡ يَاسِينَ
Maamkizi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na sifa njema kwa Ilyas
Ayah 130إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Na kama tulivyomlipa Ilyas malipo mema kwa utiifu wake, ndivyo tutakavyowalipa walio wema miongoni mwa waja wetu Waumini
Ayah 131إِنَّهُۥ مِنۡ عِبَادِنَا ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Hakika yake yeye ni miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu waliomtakasia wenye kufuata amri zake kivitendo
Ayah 132وَإِنَّ لُوطࣰ ا لَّمِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Na hakika mja wetu Lūṭ tulimchagua na tukamfanya ni miongoni mwa Mitume
Ayah 133إِذۡ نَجَّيۡنَٰهُ وَأَهۡلَهُۥٓ أَجۡمَعِينَ
Tulipomuokoa yeye na watu wa nyumbani kwake wote
Ayah 134إِلَّا عَجُوزࣰ ا فِي ٱلۡغَٰبِرِينَ
isipokuwa mkongwe aliyezeeka, naye ni mke wake, ambaye aliangamia pamoja na wale walioangamia miongoni mwa watu wake kwa ukafiri wake
Ayah 135ثُمَّ دَمَّرۡنَا ٱلۡأٓخَرِينَ
Kisha tukawaangamiza wakanushaji waliosalia miongoni mwa watu wake
Ayah 136وَإِنَّكُمۡ لَتَمُرُّونَ عَلَيۡهِم مُّصۡبِحِينَ
Na hakika yenu nyinyi, enyi watu wa Makkah mnazipitia katika safari zenu nyumba za watu wa Lūṭ na athari zao katika kipindi cha asubuhi
Ayah 137وَبِٱلَّيۡلِۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ
na pia mnazipitia katika kipindi cha usiku. Basi hamtii akilini, mkaogopa kisije kikawafika nyinyi kile kilichowafika wao
Ayah 138وَإِنَّ يُونُسَ لَمِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Hakika mja wetu Yūnus, tulimchagua na tukamfanya ni miongoni mwa Mitume
Ayah 139إِذۡ أَبَقَ إِلَى ٱلۡفُلۡكِ ٱلۡمَشۡحُونِ
Alipokimbia kutoka mji wake, akiwa na hasira juu ya watu wake, akapanda jahazi iliyojaa abiria na vyombo
Ayah 140فَسَاهَمَ فَكَانَ مِنَ ٱلۡمُدۡحَضِينَ
Mawimbi makubwa yakaizunguka jahazi hiyo kila upande. Na watu waliokuwa wamepanda jahazi wakapiga kura ili kupunguza shehena ili wasizame. Yūnus akawa ni miongoni mwa wale walioshindwa kwa kura
Ayah 141فَٱلۡتَقَمَهُ ٱلۡحُوتُ وَهُوَ مُلِيمࣱ
Hivyo basi akatupwa baharini na chewa akammeza, na hali ni kwamba Yūnus, amani imshukie, ameleta jambo la kumfanya alaumiwe
Ayah 142فَلَوۡلَآ أَنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلۡمُسَبِّحِينَ
Lau si yale yaliyotangulia kwake, ya wingi wa Ibada na matendo mema kabla ya kuingia ndani ya tumbo la chewa kwa kusema, «Hapana Mola anayepasa kuabudiwa kwa haki isipokuwa wewe, kutakasika na sifa za upungufu ni kwako, mimi nimekuwa miongoni mwa wenye kudhulumu,»
Ayah 143لَلَبِثَ فِي بَطۡنِهِۦٓ إِلَىٰ يَوۡمِ يُبۡعَثُونَ
angalikaa ndani ya tumbo la chewa, na lingalikuwa ni kaburi lake mpaka Siku ya Kiyama
Ayah 144۞فَنَبَذۡنَٰهُ بِٱلۡعَرَآءِ وَهُوَ سَقِيمࣱ
Tukamtoa kwenye tumbo la chewa na tukamtupa kwenye ardhi tupu, isiyokuwa na miti wala majengo, akiwa dhaifu wa mwili
Ayah 145وَأَنۢبَتۡنَا عَلَيۡهِ شَجَرَةࣰ مِّن يَقۡطِينࣲ
Na tukamuoteshea mmea wa matango ili umfinike na anufaike nao
Ayah 146وَأَرۡسَلۡنَٰهُ إِلَىٰ مِاْئَةِ أَلۡفٍ أَوۡ يَزِيدُونَ
Tukamtumiliza aende kwa watu wake wanaofikia elfu mia moja, bali wanazidi idadi hiyo
Ayah 147فَـَٔامَنُواْ فَمَتَّعۡنَٰهُمۡ إِلَىٰ حِينࣲ
Wakamuamini na wakafuata aliyokuja nayo kivitendo, na kwa hivyo tukawastarehesha maishani mwao mpaka wakati wa kufika ajali zao
Ayah 148فَٱسۡتَفۡتِهِمۡ أَلِرَبِّكَ ٱلۡبَنَاتُ وَلَهُمُ ٱلۡبَنُونَ
Basi waulize watu wako, ewe Mtume, «Ni vipi wamemfanya Mwenyezi Mungu ana watoto wa kike ambao wao wenyewe wanawachukia, na wao wana watoto wa kiume wanaowataka?»
Ayah 149أَمۡ خَلَقۡنَا ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ إِنَٰثࣰ ا وَهُمۡ شَٰهِدُونَ
Na waulize wao, «Je, tuliwaumba Malaika wakiwa wanawake, na hali wao wapo (wakishuhudia uumbaji huo)?»
Ayah 150أَلَآ إِنَّهُم مِّنۡ إِفۡكِهِمۡ لَيَقُولُونَ
Na miongoni mwa urongo wao ni kule kusema kwao, «Mwenyezi Mungu Amezaa
Ayah 151وَلَدَ ٱللَّهُ وَإِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ
Na kwa hakika, wao ni warongo, kwa kuwa wanakisema wasichokijua.»
Ayah 152أَصۡطَفَى ٱلۡبَنَاتِ عَلَى ٱلۡبَنِينَ
Ni kwa kitu gani Mwenyezi Mungu Achague watoto wa kike na sio wa kiume
Ayah 153مَا لَكُمۡ كَيۡفَ تَحۡكُمُونَ
Ni uamuzi mbaya sana mnaoutoa, enyi watu, wa kuwa Mwenyezi Mungu Ana watoto wa kike na nyinyi mna watoto wa kiume, na hali nyinyi hamridhiki nafsi zenu kuwa na watoto wa kike
Ayah 154أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
Je, hamkumbuki kwamba haifai wala haitakikani Awe na mtoto? Ametukuka Mwenyezi Mungu na kuwa mbali na hilo, umbali ulio juu sana
Ayah 155أَمۡ لَكُمۡ سُلۡطَٰنࣱ مُّبِينࣱ
Lakini je, mna hoja ya wazi juu ya hilo neno lenu na uzushi wenu
Ayah 156فَأۡتُواْ بِكِتَٰبِكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Iwapo mna hoja ndani ya kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu, basi kileteni, mkiwa ni wa kweli katika hilo neno lenu
Ayah 157وَجَعَلُواْ بَيۡنَهُۥ وَبَيۡنَ ٱلۡجِنَّةِ نَسَبࣰ اۚ وَلَقَدۡ عَلِمَتِ ٱلۡجِنَّةُ إِنَّهُمۡ لَمُحۡضَرُونَ
Na washirikina walifanya kuwa kuna uhusiano wa kizazi baina ya Mwenyezi Mungu na Malaika, na hakika ni kwamba Malaika washajua kuwa washirikina ni wenye kuletwa Siku ya Kiyama ili kuadhibiwa
Ayah 158سُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يَصِفُونَ
Ametakasika Mwenyezi Mungu na kila lisilofaa asifike nalo miongoni mwa yale wanaomsifu nayo washirikina
Ayah 159إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ
Lakini wale waja wa Mwenyezi Mungu wanaomtakasia katika kumuabudu hawamsifu isipokuwa kwa sifa zinazolingana na utukufu Wake, kutakasika ni Kwake
Ayah 160فَإِنَّكُمۡ وَمَا تَعۡبُدُونَ
Hakika yenu nyinyi, enyi wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kile mnachokiabudu badala ya Mwenyezi Mungu miongoni mwa waungu
Ayah 161مَآ أَنتُمۡ عَلَيۡهِ بِفَٰتِنِينَ
hamkuwa ni wenye kumpoteza yoyote
Ayah 162إِلَّا مَنۡ هُوَ صَالِ ٱلۡجَحِيمِ
isipokuwa yule Aliyemkadiria Mwenyezi Mungu aingie kwenye Moto wa Jaḥīm kwa sababu ya ukafiri wake na udhalimu wake
Ayah 163وَمَا مِنَّآ إِلَّا لَهُۥ مَقَامࣱ مَّعۡلُومࣱ
Malaika wanasema, «Hakuna yoyote miongoni mwetu isipokuwa ana makao maalumu mbinguni
Ayah 164وَإِنَّا لَنَحۡنُ ٱلصَّآفُّونَ
Na sisi ndio tunaosimama kwa kujipanga kwa safu katika kumuabudu Mwenyezi Mungu na kumtii
Ayah 165وَإِنَّا لَنَحۡنُ ٱلۡمُسَبِّحُونَ
Na sisi ndio tunaomtakasa Mwenyezi Mungu na kila kisichofaa kunasibishwa nacho.»
Ayah 166وَإِن كَانُواْ لَيَقُولُونَ
Na hakika makafiri wa Makkah walikuwa wakisema kabla hujatumilizwa
Ayah 167لَوۡ أَنَّ عِندَنَا ذِكۡرࣰ ا مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ
«Ewe Mtume! Lau vingalitujia vitabu na Manabii vile vilivyowajia wa mwanzo kabla yetu
Ayah 168لَكُنَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ
tungalikuwa waja wa Mwenyezi Mungu wakweli katika Imani, waliotakaswa kwa kufanya Ibada.»
Ayah 169فَكَفَرُواْ بِهِۦۖ فَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ
Ulipowajia wao utajo wa watu wa mwanzo na utajo wa watu wa mwisho na kitabu kikamilifu kabisa na bora wa Mitume, naye ni Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, walimkanusha. Basi wataijua adhabu watakayopatiwa Siku ya Mwisho
Ayah 170وَلَقَدۡ سَبَقَتۡ كَلِمَتُنَا لِعِبَادِنَا ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Kwa hakika lishatangulia neno letu, ambalo halina namna ya kurudi, la kuwaahidi waja wetu waliopewa utume
Ayah 171إِنَّهُمۡ لَهُمُ ٱلۡمَنصُورُونَ
kwamba watapata usaidizi juu ya maadui zao, kwa hoja na nguvu
Ayah 172وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ ٱلۡغَٰلِبُونَ
na kwamba askari wetu wanaopigana jihadi katika njia yetu ndio wenye kuwashinda maadui zao kila mahali, kuzingatia mwishoni na marejeo
Ayah 173فَتَوَلَّ عَنۡهُمۡ حَتَّىٰ حِينࣲ
Basi wape mgongo, ewe Mtume, wale walioshindana na wasiikubali haki mpaka ukamalizika muda waliopatiwa muhula na ikaja amri ya Mwenyezi Mungu ya wao kuadhibiwa
Ayah 174وَأَبۡصِرۡهُمۡ فَسَوۡفَ يُبۡصِرُونَ
wangojee na subiri uone: ni adhabu gani itakayowashukia wao kwa kuenda kinyume nawe? Basi wataiona adhabu ya Mwenyezi Mungu itakayowashukia
Ayah 175أَفَبِعَذَابِنَا يَسۡتَعۡجِلُونَ
Je kuteremkiwa kwao na adhabu yetu ndilo jambo wanalokuharakishia, ewe Mtume
Ayah 176فَإِذَا نَزَلَ بِسَاحَتِهِمۡ فَسَآءَ صَبَاحُ ٱلۡمُنذَرِينَ
Basi adhabu yetu itakapowashukia, asubuhi mbaya zaidi ni asubuhi yao
Ayah 177وَتَوَلَّ عَنۡهُمۡ حَتَّىٰ حِينࣲ
Na uwape mgongo mpaka Mwenyezi Mungu Atoe idhini ya wao kuadhibiwa
Ayah 178وَأَبۡصِرۡ فَسَوۡفَ يُبۡصِرُونَ
Na uwangojee, kwani wataiona adhabu itakayowashukia na mateso
Ayah 179سُبۡحَٰنَ رَبِّكَ رَبِّ ٱلۡعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ
Mola wa enzi na utukufu Ameepukana na kuwa juu ya kila kile ambacho wanaomzulia urongo wanamsifu nacho
Ayah 180وَسَلَٰمٌ عَلَى ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Na maamkizi ya Mwenyezi Mungu ya daima,sifa Zake na amani Yake ziwafikie Mitume wote
Ayah 181وَٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Na shukrani na sifa njema ni za Mola wa viumbe wote ulimwenguni na Akhera. Yeye Ndiye Mstahiki wa hilo Peke Yake, Hana mshirika Wake
Ayah 182