Surah Adh-Dhaariyat — The Winnowing Winds
Surah Adh-Dhaariyat (The Winnowing Winds) — 51/114 · 60 aya. Soma na usikilize kwa maandishi ya Kiarabu na tafsiri ya Kiswahili.
وَٱلذَّٰرِيَٰتِ ذَرۡوࣰ ا
Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Anaapa kwa upepo wenye kurusha mchanga
Ayah 1فَٱلۡحَٰمِلَٰتِ وِقۡرࣰ ا
na mawingu yenye kubeba uzito mkubwa wa maji
Ayah 2فَٱلۡجَٰرِيَٰتِ يُسۡرࣰ ا
na jahazi zinazopita baharini na kutembea kwa upesi na usahali
Ayah 3فَٱلۡمُقَسِّمَٰتِ أَمۡرًا
na Malaika wenye kugawanya amri za Mwenyezi Mungu kwa viumbe Vyake
Ayah 4إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِقࣱ
kwamba mnayoahidiwa, enyi watu, ya kufufuliwa na kuhesabiwa ni tukio lenye kuwa kwa kweli na yakini
Ayah 5وَإِنَّ ٱلدِّينَ لَوَٰقِعࣱ
na kwamba kuhesabiwa na kulipwa mema kwa amali njema ni jambo lisilo na budi
Ayah 6وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلۡحُبُكِ
Na Anaapa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa mbingu zenye umbo zuri, kwamba nyinyi, enyi wakanushaji
Ayah 7إِنَّكُمۡ لَفِي قَوۡلࣲ مُّخۡتَلِفࣲ
mko kwenye neno linalogongana kuhusu Qur’ani na kuhusu Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie
Ayah 8يُؤۡفَكُ عَنۡهُ مَنۡ أُفِكَ
Anaepushwa na Qur’ani na Mtume yule aliyeepushwa na lile la kuviamini hivyo viwili kwa kuzipa mgongo dalili za Mwenyezi Mungu na hoja Zake za yakini, na kwa hivyo haafikiwi kwenye kheri
Ayah 9قُتِلَ ٱلۡخَرَّٰصُونَ
Wamelaaniwa warongo wenye dhana zisizo za kweli
Ayah 10ٱلَّذِينَ هُمۡ فِي غَمۡرَةࣲ سَاهُونَ
waliomo ndani ya dimbwi la ukafiri na upotevu hali ya kuwa wameghafilika na kujikita kwenye ubatilifu wao
Ayah 11يَسۡـَٔلُونَ أَيَّانَ يَوۡمُ ٱلدِّينِ
Wanauliza hawa wenye kukanusha suali la kuonyesha kuwa ni jambo lisilowezekana na la kuonyesha ukanushaji, «Ni lini Siku ya kuhesabiwa na kulipwa?»
Ayah 12يَوۡمَ هُمۡ عَلَى ٱلنَّارِ يُفۡتَنُونَ
Siku ya Malipo ni Siku ya wao kuadhibiwa kwa kuchomwa kwa Moto na waambiwe
Ayah 13ذُوقُواْ فِتۡنَتَكُمۡ هَٰذَا ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تَسۡتَعۡجِلُونَ
«Onjeni adhabu yenu ambayo mlikuwa mkiifanyia haraka duniani.»
Ayah 14إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّٰتࣲ وَعُيُونٍ
Hakika ya wale wanaomcha Mwenyezi Mungu watakuwa kwenye mabustani ya Pepo makubwa na chemchemi za maji yenye kutembea. Mwenyezi Mungu Atawapa yote wanayoyatamani ya aina mbalimbali za starehe
Ayah 15ءَاخِذِينَ مَآ ءَاتَىٰهُمۡ رَبُّهُمۡۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَبۡلَ ذَٰلِكَ مُحۡسِنِينَ
Watazipokea neema hizo wakiwa wameridhika nazo na nafsi zao zina furaha. Hakika wao, kabla ya kupata sterehe hizo, walikuwa wema duniani kwa matendo yao mema
Ayah 16كَانُواْ قَلِيلࣰ ا مِّنَ ٱلَّيۡلِ مَا يَهۡجَعُونَ
Wema hawa walikuwa wakilala kipindi kichache usiku, wakiswali kwa Mola wao wakimnyenyekea
Ayah 17وَبِٱلۡأَسۡحَارِ هُمۡ يَسۡتَغۡفِرُونَ
na katika nyakati za mwisho wa usiku, kabla ya alfajiri kwa muda mchache, walikuwa wakimuomba Mwenyezi Mungu msamaha wa dhambi zao
Ayah 18وَفِيٓ أَمۡوَٰلِهِمۡ حَقࣱّ لِّلسَّآئِلِ وَٱلۡمَحۡرُومِ
Na katika mali yao kulikuwa na haki ya lazima na ya kupendekezwa kupewa wahitaji wanaowaomba watu na wasiowaomba kwa kuona haya
Ayah 19وَفِي ٱلۡأَرۡضِ ءَايَٰتࣱ لِّلۡمُوقِنِينَ
Na katika ardhi kuna mazingatio na dalili waziwazi za uweza wa Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mola wa haki, Aliye Peke Yake na asiye na mshirika, na wenye kumuamini Mtume Wake. rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie
Ayah 20وَفِيٓ أَنفُسِكُمۡۚ أَفَلَا تُبۡصِرُونَ
Na katika kuwaumba nyinyi kuna dalili za uweza wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, na kuna mazingatio ya kuwaonyesha nyinyi upweke wa Muumba wenu na kwamba Yeye hakuna Mola Anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye. Je, mumeghafilika na hilo mkawa hamlioni mkazingatia kwalo
Ayah 21وَفِي ٱلسَّمَآءِ رِزۡقُكُمۡ وَمَا تُوعَدُونَ
Na mbinguni kuna riziki yenu na yale mnayoahidiwa ya kheri na shari, na thawabu na mateso na yasiyokuwa hayo. Yote yameandikwa na kukadiriwa
Ayah 22فَوَرَبِّ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ إِنَّهُۥ لَحَقࣱّ مِّثۡلَ مَآ أَنَّكُمۡ تَنطِقُونَ
Anaapa Mwenyezi Mungu kwa dhati Yake tukufu kwamba kile Alichowaahidi ni kweli, msikifanyie shaka kama ambavyo hamshuku kuwa nyinyi mnasema
Ayah 23هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ضَيۡفِ إِبۡرَٰهِيمَ ٱلۡمُكۡرَمِينَ
Je imekujia wewe, ewe Mtume, habari ya wageni wa Ibrāhīm aliyewakirimu
Ayah 24إِذۡ دَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَقَالُواْ سَلَٰمࣰ اۖ قَالَ سَلَٰمࣱ قَوۡمࣱ مُّنكَرُونَ
na walikuwa ni miongoni mwa Malaika watukufu- wakati walipomjia nyumbani kwake, wakamwamkia kwa kumwambia, «Salama!»Akawarudishia maamkizi kwa kusema, «Salama ni kwenu! Nyinyi ni watu wageni hatuwajui.»
Ayah 25فَرَاغَ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ فَجَآءَ بِعِجۡلࣲ سَمِينࣲ
Akaondoka kwa siri na akaelekea kwa watu wa nyumbani kwake akamlenga ndama mnono akamchinja, akamchoma
Ayah 26فَقَرَّبَهُۥٓ إِلَيۡهِمۡ قَالَ أَلَا تَأۡكُلُونَ
kisha akamuweka mbele yao na akawakaribisha kwa upole kwa kusema, «Si mle»
Ayah 27فَأَوۡجَسَ مِنۡهُمۡ خِيفَةࣰۖ قَالُواْ لَا تَخَفۡۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَٰمٍ عَلِيمࣲ
Alipowaona hawali aliingiwa na kicho cha kuwaogopa, na hapo wakamwambia, «Usiogope! Sisi ni wajumbe wa Mwenyezi Mungu. Na wakampa bishara kwamba mkewe Sarah atamzalia mtoto atakayekuwa ni miongoni mwa watu wanaomjua Mwenyezi Mungu na kuijua Dini Yake, naye ni Isḥāq, amani imshukie
Ayah 28فَأَقۡبَلَتِ ٱمۡرَأَتُهُۥ فِي صَرَّةࣲ فَصَكَّتۡ وَجۡهَهَا وَقَالَتۡ عَجُوزٌ عَقِيمࣱ
Aliposikia mke wa Ibrāhīm maneno ya bishara ya hao Malaika, alielekea upande wao na ukelele, akajipiga uso wake kwa kulionea ajabu jambo hili na akasema, «Vipi nitazaa na mimi ni tasa sizai?»
Ayah 29قَالُواْ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡعَلِيمُ
Malaika wa Mwenyezi Mungu wakamwambia, «Hivyo ndivyo Alivyosema Mola wako kama tulivyokwambia. Na Yeye Muweza wa hilo, hapana la ajabu kutokana na uweza Wake. Hakika Yeye, Aliyetakasika na kutukuka, Ndiye Mwenyew hekima Anayeviweka vitu mahali pake, Ndiye Mwenye kuyajua maslahi ya waja Wake
Ayah 30۞قَالَ فَمَا خَطۡبُكُمۡ أَيُّهَا ٱلۡمُرۡسَلُونَ
Akasema Ibrāhīm, amani imshukie, kuwaambia Malaika wa Mwenyezi Mungu «Mna jambo gani na mmetumwa na ujumbe gani
Ayah 31قَالُوٓاْ إِنَّآ أُرۡسِلۡنَآ إِلَىٰ قَوۡمࣲ مُّجۡرِمِينَ
Wakasema, «Mwenyezi Mungu Ametutuma tuende kwa watu waliofanya uhalifu kwa kumkanusha Mwenyezi Mungu
Ayah 32لِنُرۡسِلَ عَلَيۡهِمۡ حِجَارَةࣰ مِّن طِينࣲ
ili tuwaangamize kwa mawe ya udongo uliokuwa mkavu kama mawe
Ayah 33مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ لِلۡمُسۡرِفِينَ
uliotiwa alama kutoka kwa Mola wako ya hawa waliokiuka mpaka katika uchafu na uasi
Ayah 34فَأَخۡرَجۡنَا مَن كَانَ فِيهَا مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Tukamtoa kila aliyekuwa kwenye mji wa watu wa Lūṭ katika watu walioamini
Ayah 35فَمَا وَجَدۡنَا فِيهَا غَيۡرَ بَيۡتࣲ مِّنَ ٱلۡمُسۡلِمِينَ
Hatukupata kwenye mji huo isipokuwa nyumba moja ya Waislamu, nayo ni nyumba ya Lūṭ, amani imshukie
Ayah 36وَتَرَكۡنَا فِيهَآ ءَايَةࣰ لِّلَّذِينَ يَخَافُونَ ٱلۡعَذَابَ ٱلۡأَلِيمَ
Na tukaacha kwenye mji huo uiliotajwa athari iliyosalia ya adhabu iwe ni alama ya uweza wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na vile alivyowatesa makafiri. Ili hilo liwe ni zingatio kwa wale wanaoiogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu iliyo kali na yenye kuumiza
Ayah 37وَفِي مُوسَىٰٓ إِذۡ أَرۡسَلۡنَٰهُ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ بِسُلۡطَٰنࣲ مُّبِينࣲ
Na katika kumtumiliza kwetu Mūsā, aende kwa Fir'awn na wakuu wa utawala wake, kwa aya na miujiza yenye kushinda, kuna alama kwa wanaoogopa adhabu kali
Ayah 38فَتَوَلَّىٰ بِرُكۡنِهِۦ وَقَالَ سَٰحِرٌ أَوۡ مَجۡنُونࣱ
Fir'awn akayapa mgongo akighurika nguvu zake na wasaidizi wake na akasema kuhusu Mūsā, «Yeye ni mchawi au ni mwendawazimu,»
Ayah 39فَأَخَذۡنَٰهُ وَجُنُودَهُۥ فَنَبَذۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡيَمِّ وَهُوَ مُلِيمࣱ
Tukamchukua Fir'awn na askari wake tukawatupa baharini, na hali ameleta jambo la kulaumiwa kwa sababu ya ukafiri wake, kukanusha kwake na ubaya wake
Ayah 40وَفِي عَادٍ إِذۡ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمُ ٱلرِّيحَ ٱلۡعَقِيمَ
Na kuhusu mambo ya watu wa kabila la 'Ād na kuwaangamiza wao kuna dalili na mazingatio kwa mwenye kutia mambo akilini, tulipowapelekea wao upepo usiokuwa na baraka na usioleta kheri yoyote
Ayah 41مَا تَذَرُ مِن شَيۡءٍ أَتَتۡ عَلَيۡهِ إِلَّا جَعَلَتۡهُ كَٱلرَّمِيمِ
hauachi kitu chochote unachokipitia isipokuwa hukifanya ni kama kitu kilichochakaa
Ayah 42وَفِي ثَمُودَ إِذۡ قِيلَ لَهُمۡ تَمَتَّعُواْ حَتَّىٰ حِينࣲ
Na kuhusu watu wa kabila la Thamūd na kuangamizwa kwao kuna dalili na mazingatio, walipoambiwa-na msemaji hapa ni Nabii wao Ṣāliḥ, amani imshukie-, «Jistarehesheni mjini kwenu siku tatu mpaka muda wenu wa kuishi ukome
Ayah 43فَعَتَوۡاْ عَنۡ أَمۡرِ رَبِّهِمۡ فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّٰعِقَةُ وَهُمۡ يَنظُرُونَ
Wakaasi amri ya Mola wao, wakapatikana na ukelele wa adhabu, na huku wanayaangalia mateso yao kwa macho yao
Ayah 44فَمَا ٱسۡتَطَٰعُواْ مِن قِيَامࣲ وَمَا كَانُواْ مُنتَصِرِينَ
Haikumkinika wao kukimbia wala kusimama kwa adhabu waliokuwa nayo, na hawakuwa ni wenye kujitetea nafsi zao
Ayah 45وَقَوۡمَ نُوحࣲ مِّن قَبۡلُۖ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَوۡمࣰ ا فَٰسِقِينَ
Na tuliwaangamiza watu wa Nūḥ kabla ya hawa, hakika wao walikuwa ni watu wenye kuenda kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu, wenye kutoka nje ya utiifu Kwake
Ayah 46وَٱلسَّمَآءَ بَنَيۡنَٰهَا بِأَيۡيْدࣲ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ
Na mbingu tuliziumba na tukazitengeneza vizuri, na tukazifanya ni sakafu ya ardhi kwa nguvu na uweza mkubwa, na sisi tutayapanua maeneo yake na pande zake
Ayah 47وَٱلۡأَرۡضَ فَرَشۡنَٰهَا فَنِعۡمَ ٱلۡمَٰهِدُونَ
Na ardhi tuliifanya ni tandiko la viumbe wapate kutulia juu yake, Basi bora wa wenye kutandika ni sisi
Ayah 48وَمِن كُلِّ شَيۡءٍ خَلَقۡنَا زَوۡجَيۡنِ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ
Na kutokana na kila kitu katika jinsi ya vitu vilivyoko tumeumba aina mbili tafauti, ili mjikumbushe uweza wa Mwenyezi Mungu na mzingatie
Ayah 49فَفِرُّوٓاْ إِلَى ٱللَّهِۖ إِنِّي لَكُم مِّنۡهُ نَذِيرࣱ مُّبِينࣱ
Basi kimbieni, enyi watu , kutoka kwenye mateso ya Mwenyezi Mungu na muelekee kwenye rehema Yake kwa kumuamini Yeye na Mtume Wake, kufuata amri Yake na kufanya mambo ya utiifu Kwake. Hakika mimi, kwenu nyinyi, ni muonyaji ambaye maonyo yake yako waziwazi. Na Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, alikuwa akizungukwa na mambo hukimbilia Swala, na huku ndiko kumkimbilia Mwenyezi Mungu
Ayah 50وَلَا تَجۡعَلُواْ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَۖ إِنِّي لَكُم مِّنۡهُ نَذِيرࣱ مُّبِينࣱ
Na msimfanye pamoja na Mwenyezi Mungu muabudiwa mwingine, Hakika mimi kwenu nyinyi ni muonyaji amabaye uonyaji wake uko waziwazi
Ayah 51كَذَٰلِكَ مَآ أَتَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا قَالُواْ سَاحِرٌ أَوۡ مَجۡنُونٌ
Kama walivyomkanusha Makureshi Mtume wao Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wakasema, «Yeye ni mshairi, au mchawi, au mwendawazimu.», ndivyo walivyofanya ummah waliowakanusha Mitume wao kabla ya Makureshi, na Mwenyezi Mungu Akawashushia mateso Yake
Ayah 52أَتَوَاصَوۡاْ بِهِۦۚ بَلۡ هُمۡ قَوۡمࣱ طَاغُونَ
Je, waliusiana wa mwanzo na wa mwisho kumkanusha Mtume waliposema hivyo kwa umoja wao? Bali wao ni watu wenye kukiuka mipaka kwa uhalifu, nyoyo zao zimefanana na vitendo vyao kwa ukafiri na ukiukaji mipaka, ndipo waliokuja nyuma wakasema hayo kama walivyosema waliotangulia
Ayah 53فَتَوَلَّ عَنۡهُمۡ فَمَآ أَنتَ بِمَلُومࣲ
Wapuuze hao washirikina, ewe Mtume, mpaka itakapokujia wewe amri ya Mwenyezi Mungu kuhusu wao, hapatakuwa na yoyote mwenye kukulaumu, kwani ushafikisha yale uliyotumilizwa kwayo
Ayah 54وَذَكِّرۡ فَإِنَّ ٱلذِّكۡرَىٰ تَنفَعُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Pamoja na kuwapuuza wao, ewe Mtume, na kutoshughulika na ufidhuli wao, endelea kuwaidhia wale uliotumilizwa kwao, kwani kukumbusha na kuwaidhia watanufaika nako wale wenye nyoyo zenye kuamini, na katika kufanya mawili hayo kuna kusimamisha hoja kwa wenye kupa mgongo
Ayah 55وَمَا خَلَقۡتُ ٱلۡجِنَّ وَٱلۡإِنسَ إِلَّا لِيَعۡبُدُونِ
Na sikuumba majini na binadamu na kutumiliza Mitume wote isipokuwa kwa lengo tukufu, nalo niabudiwe mimi Peke Yangu, na sio asiyekuwa mimi
Ayah 56مَآ أُرِيدُ مِنۡهُم مِّن رِّزۡقࣲ وَمَآ أُرِيدُ أَن يُطۡعِمُونِ
Sitaki kutoka kwao riziki wala sitaki wanilishe, kwani mimi Ndiye Mpaji Mwenye kuruzuku. Kwani Yeye, Aliyetakasika na kila sifa za upungufu, hawahitaji viumbe Vyake, bali wao ndio wahitaji Kwake katika hali zao zote, Yeye Ndiye Mwenye kuwaumba na kuwaruzuku na Aliyejikwasisha nao kwa kutowahitajia
Ayah 57إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلرَّزَّاقُ ذُو ٱلۡقُوَّةِ ٱلۡمَتِينُ
Hakika Mwenyezi Mungu , Peke Yake, Ndiye Mwenye kuviruzuku viumbe Vyake, Ndiye Anayedhamini chakula chao, Mwenye nguvu Aliye Thabiti, Hatendeshwi nguvu wala hakuna Mwenye kushindana Naye. Ni Wake Yeye uweza wote na nguvu
Ayah 58فَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُواْ ذَنُوبࣰ ا مِّثۡلَ ذَنُوبِ أَصۡحَٰبِهِمۡ فَلَا يَسۡتَعۡجِلُونِ
Hakika wale waliodhulumu kwa kumkanusha kwao Mtume Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wana fungu la adhabu ya Mwenyezi Mungu mfano wa fungu la wenzi wao waliopita kabla yao. Basi wasiifanyie haraka adhabu , kwani hapana budi ni yenye kuwajia
Ayah 59فَوَيۡلࣱ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن يَوۡمِهِمُ ٱلَّذِي يُوعَدُونَ
maangamivu na usumbufu ni wa wale waliomkanusha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, kutokana na Siku yao wanayoahidiwa kuteremkiwa na adhabu, nayo ni Siku ya Kiyama
Ayah 60