Surah At-Takaathur — Competition

Surah At-Takaathur (Competition) — 102/114 · 8 aya. Soma na usikilize kwa maandishi ya Kiarabu na tafsiri ya Kiswahili.

أَلۡهَىٰكُمُ ٱلتَّكَاثُرُ

Kumewashughulisha kujifahiri kwa mali na watoto mkawacha kumtii Mwenyezi Mungu

Ayah 1

حَتَّىٰ زُرۡتُمُ ٱلۡمَقَابِرَ

Kujishughulisha kwenu na hilo kumeendelea mpaka mkawa makaburini na mkazikwa humo

Ayah 2

كَلَّا سَوۡفَ تَعۡلَمُونَ

Siyo namna hii inatakiwa iwapumbaze kushindana kwa wingi wa mali. Itawadhihirikia kuwa Nyumba ya Akhera ni bora kwenu

Ayah 3

ثُمَّ كَلَّا سَوۡفَ تَعۡلَمُونَ

Kisha tahadharini mtajua mwisho mbaya wa kutojishughulisha na Akhera

Ayah 4

كَلَّا لَوۡ تَعۡلَمُونَ عِلۡمَ ٱلۡيَقِينِ

Siyo namna hii inatakiwa iwashughulishe kushindana kwa wingi wa mali.Lau mnajua kikweli, mngalirudi nyuma na mngaliangusiliza kuokoa nafsi zenu kutoka kwenye maangamivu

Ayah 5

لَتَرَوُنَّ ٱلۡجَحِيمَ

Mtauona Moto

Ayah 6

ثُمَّ لَتَرَوُنَّهَا عَيۡنَ ٱلۡيَقِينِ

Kisha mtauona bila shaka

Ayah 7

ثُمَّ لَتُسۡـَٔلُنَّ يَوۡمَئِذٍ عَنِ ٱلنَّعِيمِ

Kisha mtaulizwa kuhusu kila aina ya starehe mliyokuwa nayo

Ayah 8