Surah Al-Masad — The Palm Fibre
Surah Al-Masad (The Palm Fibre) — 111/114 · 5 aya. Soma na usikilize kwa maandishi ya Kiarabu na tafsiri ya Kiswahili.
تَبَّتۡ يَدَآ أَبِي لَهَبࣲ وَتَبَّ
Imehasirika mikono miwili ya Abu Lahab, na yeye mwenyewe ameangamia, kwa kumuudhi Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. Hasara ya Abu Lahab ilithubutu
Ayah 1مَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُ مَالُهُۥ وَمَا كَسَبَ
Hayakumfalia kitu mali yake na watoto wake. Kwani hivyo havitamkinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu pindi ikimshukia
Ayah 2سَيَصۡلَىٰ نَارࣰ ا ذَاتَ لَهَبࣲ
Ataingia kwenye Moto wenye kuroroma
Ayah 3وَٱمۡرَأَتُهُۥ حَمَّالَةَ ٱلۡحَطَبِ
yeye na mke wake ambaye alikuwa akibeba miba na kuiweka kwenye njia anayopita Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ili kumuudhi
Ayah 4فِي جِيدِهَا حَبۡلࣱ مِّن مَّسَدِۭ
Kwenye shingo yake patakuwa na kamba imara ya lifu gumu lilio kavu; atabebewa nayo kwenye Moto wa Jahanamu, kisha atarushwa nayo mpaka chini
Ayah 5